Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za kulevya
Christofa Shekiondo akifafanua jambo wakati wa kilele cha maadhimisho ya
ya kitaifa ya siku ya kupiga vita Dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika
Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu [Sera , Uratibu na Bunge]
Willam Lukuvi akielezea jambo wakati alipokuwa akufunga maadhimisho ya
kilele cha kupiga vita madawa ya kulevya yaliyofanyika Dodoma jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge] William
Lukuvi akipewa maelekezo ya Aina ya Madawa ya kulevya na Mkemia mkuu wa
Serikali Profesa Samweli Manyere alipotembelea Maonyesho hayo baada ya
kuyafunga Dodoma jana.
Wananchi mwa mkoa wa Dodoma wakiandamana kuelekea Viwanja vya nyerere
[Nyerere Squere] kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku
ya kupiga vita vita Dawa za kulevya yaliyifanyika jana.
Na John Banda,
Dodoma
SELIKARI
imesema tatizo la uingiaji na utumiaji wa madawa ya kulevya ni kubwa nchini
kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa makundi mbali mbali hasa kundi la
vijana.
Hayo yalisemwa
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge] William Lukuvi
kwenye kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita Dawa za kulevya yaliyofanyika jana
Dodoma.
Lukuvi
alisema katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la watanzania
wanaojiingiza katka biashara haramu ya Dawa za kulevya, hali inayosababisha
changamoto kwa nchi katika kuabiliana na madhara ya biashara hiyo.
Alisema kwa
mujibu wa takwimu za vyombo vya Dola, Viwango vya Heroin na Cocaine vilivyoendelea
kukamatwa nchini kuanzia mwaka 2010 ni vikubwa kuliko vile vilivyokamatwa miaka
10 iliyopita.
‘’Mwaka huu
pee kumekuwa na ukamatwaji mkubwakatika eneo la kimataifa bahari ya hindi
karibu na nchi yetu ambapo jumla ya kilo 914 za Heroin zilikamatwa na kikosi
kazi cha kuzuia uharamia cha jeshi la kimataifa, mfano huu unaonyesha uwezekano
wa dawa hizi kuingizwa kwa wingi nchi’’, Alisema Lukuvi
Aidha Waziri
huyo aliongeza kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la watanzania wanaijiingiza katika
biashara ya Dawa za kulevya na wanaifanya ndani na nje ya mipaka ya nchi kwa
mfano kipindi cha mwaka 2008/12 jumla ya watuhumiwa 10, 799 walikamatwa.
Alisema vilevile
wengine 240 walikamatwa katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil, Paksitan na
Africa ya kusini hali hii inaharibu taswila ya nchi na inasababisha watanzania
wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda
nchi mbalimbali Duniani.
Lukuvu
alionya kuwa zipo Dalili kuwa biashara hii haramu ikiachwa iendelee athari kama
kuingiliwa kwa misingi ya kiutawara na wafanyabiashara hiyo kwa masrahi yao
binafsi, kuongezeka kwa waathirika wa Rushwa pia kuwa na mzunguko wa fedha
haramu na mfumuko wa bei.
Kwa upande
wake Kamishina wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya Nchini Christofa
Shekiondo alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la Dawa za kulevya zinazozalishwa
nje nchi aina ya Heroin na Cocain kuanzia 2009 hadi sasa.
Shekiondo
alitaja takwimu kuwa tangu mwaka 2008 walipokamata Dawa za kulevya aina ya
Heroin kilo 3, Cocain kilo 4, Bhangi KG 76, 400, mirungi kg 5,332 na kufikia
mwezi wa machi 2013 jumla ya kg za Heroin ni 754.57, Cocain kg 35630, Bhangi kg
210,335.80 na mirungi kg 44,570. 80