MADAWA YA KULEVYA YAKITHIRI NCHINI

Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za kulevya Christofa Shekiondo akifafanua jambo wakati wa kilele cha maadhimisho ya ya kitaifa ya siku ya kupiga vita Dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu [Sera , Uratibu na Bunge] Willam Lukuvi akielezea jambo wakati alipokuwa akufunga maadhimisho ya kilele cha kupiga vita madawa ya kulevya yaliyofanyika Dodoma jana.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge] William Lukuvi akipewa maelekezo ya Aina ya Madawa ya kulevya na Mkemia mkuu wa Serikali Profesa Samweli Manyere alipotembelea Maonyesho hayo baada ya kuyafunga Dodoma jana.
Wananchi mwa mkoa wa Dodoma wakiandamana kuelekea Viwanja vya nyerere [Nyerere Squere] kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita vita Dawa za kulevya yaliyifanyika jana.
 Na John Banda, Dodoma

SELIKARI imesema tatizo la uingiaji na utumiaji wa madawa ya kulevya ni kubwa nchini kiasi cha kusababisha madhara makubwa kwa makundi mbali mbali hasa kundi la vijana.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge] William Lukuvi kwenye kilele cha Maadhimisho ya kupiga vita Dawa za kulevya yaliyofanyika jana Dodoma.

Lukuvi alisema katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la watanzania wanaojiingiza katka biashara haramu ya Dawa za kulevya, hali inayosababisha changamoto kwa nchi katika kuabiliana na madhara ya biashara hiyo.

Alisema kwa mujibu wa takwimu za vyombo vya Dola, Viwango vya Heroin na Cocaine vilivyoendelea kukamatwa nchini kuanzia mwaka 2010 ni vikubwa kuliko vile vilivyokamatwa miaka 10 iliyopita.

‘’Mwaka huu pee kumekuwa na ukamatwaji mkubwakatika eneo la kimataifa bahari ya hindi karibu na nchi yetu ambapo jumla ya kilo 914 za Heroin zilikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia uharamia cha jeshi la kimataifa, mfano huu unaonyesha uwezekano wa dawa hizi kuingizwa kwa wingi nchi’’, Alisema Lukuvi

Aidha Waziri huyo aliongeza kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la watanzania wanaijiingiza katika biashara ya Dawa za kulevya na wanaifanya ndani na nje ya mipaka ya nchi kwa mfano kipindi cha mwaka 2008/12 jumla ya watuhumiwa 10, 799 walikamatwa.

Alisema vilevile wengine 240 walikamatwa katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil, Paksitan na Africa ya kusini hali hii inaharibu taswila ya nchi na inasababisha watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali Duniani.   

Lukuvu alionya kuwa zipo Dalili kuwa biashara hii haramu ikiachwa iendelee athari kama kuingiliwa kwa misingi ya kiutawara na wafanyabiashara hiyo kwa masrahi yao binafsi, kuongezeka kwa waathirika wa Rushwa pia kuwa na mzunguko wa fedha haramu na mfumuko wa bei.

Kwa upande wake Kamishina wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya Nchini Christofa Shekiondo alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la Dawa za kulevya zinazozalishwa nje nchi aina ya Heroin na Cocain kuanzia 2009 hadi sasa.

Shekiondo alitaja takwimu kuwa tangu mwaka 2008 walipokamata Dawa za kulevya aina ya Heroin kilo 3, Cocain kilo 4, Bhangi KG 76, 400, mirungi kg 5,332 na kufikia mwezi wa machi 2013 jumla ya kg za Heroin ni 754.57, Cocain kg 35630, Bhangi kg 210,335.80 na mirungi kg 44,570. 80


No comments:

Post a Comment