Na John Banda,Dodoma.
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma imesema elimu
inayotolewa na vyombo vya habari kuhusu kuwafichua wahamiaji haramu
wanaoingia nchini kinyemela bila kibali halali.
Imefanikiwa kutokana na mahusiano mazuri na Halmashari ambazo zimeamua
kutekeleza kwa kuziangiza ngazi zote za vijiji,kata hadi tarafa ziwe na kitabu
cha kuhodheresha wageni wote wanaoingia katika maeneo yao.
hayo yamesemwa na Naibu
Kamishana wa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Norah Masawe alipokuwa akivishukuru vyombo
vya habari, kwa kushirikiana
katika utoaji wa taarifa ya elimu inayotolewa na idara hiyo kwa taasisi,mashirika
na wakazi wa mkoa huo.
Norah alisema elimu hiyo inayotolewa
kwa kupitia vyombo vya habari,aidha imeleta mwitikio kwa watendaji wa ngazi zote
za serikali na wananchi kuwa na utayari wa kwenda mahakamani kutoa ushahidi tofauti
na kipindi cha miaka ya nyuma.
Naibu Kamishana huyo alisema kuwa hivi
sasa elimu hiyo inayotolewa na Idara hiyo ya Uhamiaji imeweza kuzifanya
Halmashauri kuangiza watendaji wake kuwa na kitabu cha kuandikisha wageni
wanaoingia kwa lengo la kuwabaini wahamiaji haramu.
Alisema hivi sasa watendaji kwa
kushirikiana na wananchi wanashirikiana na Idara ya Uhamiaji katika kuwabaini watu
wanaoingia nchini kinyemela na kuamua kukaa nchini huku wengine wakijishughulisha
na kazi mbalimbali bila kibali halali.
“Unajua hapo mwanzo utaratibu huu
ulikuwepo kwa kila balozi wa nyumba kumi alikuwa na kitabu cha kuhodheresha
wageni wanaoingia katika maeneo yao
na ndivyo inavyotakiwa kwa hivi sasa kwa hali hiyo ili kuwabaini wahamiaji
haramu”alisema Norah.
Norah alisema kuwa Mkoa wa Dodoma
umekuwa na matukio mengi ya uingiaji wahamiaji haramu na hatimaye kufanikisha
kuwakamata,hii inatokana na wakazi hao kuwa na mahusiano mazuri baada ya
kupatiwa elimu ya jinsi ya kuwatambua wageni hao.
Aidha Naibu huyo wa idara ya uhamiaji ameendelea kuwataka
wananchi wa mkoa huo kutoa ushirikiano katika kuwatambua wahamiaji hao haramu kwa
kuwa watu hao wanaishi kwenye maeneo yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment