Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
David Misime akizungumza na viongozi wa madhehebu ya dini ofisini kwake
alipowaita ili kujenga mahusiano ya kimawasiriano.
(PICHA NA JOHN BANDA)
Na John Banda,Dodoma.
JESHI la Polisi Mkoani Dodoma imewaomba
viongozi wa madhehebu ya dini kushirikiana katika mawasiliano ili kubaini uhalifu
na wahalifu.
Ombi hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi
Mkoani hapa David Misime, alipokuwa akizungumza na viongozi wa madhehebu ya
dini ya Kiislamu na Kikristo alipowaita ofisini kwake ili kujenga mahusiano
kati yao.
Miseme alisema viongozi wa madhehebu
ya dini wapo karibu na jamii,hivyo wanayo
fursa kubwa ya kuweza kubaini
uhalifu na wahalifu
Aidha kamanda huyo wa polisi amewasisitiza
viongozi hao kuendelea kufanya doria za kiroho maana wakifanya hivyo uharifu
utapungua nchini na waumini wao watapata
baraka na thwawabu,maana kwa upande wao
polisi wanafanya doria za kimwili.
Misime ameongeza kwa kuwataka viongozi
hao kuendelea kuhubiri utii wa sheria
bila shuruti kutokana na wao kuwa karibu na wananchi kwa kuwa maana wakiitii sheria hiyo hata
ajali za barabarani ambazo zimekuwa zinasababishwa na uzembe zitapugua
“Mimi ninawaheshimu sana viongozi wa
dini kwa sababu wao ndiyo wanachangia utulivu uliopo nchini,na hata mimi ikiwa
wataniona na kosa lolote wasisite kuniita na kunionya kama walivyokuwa
wakifanya zamani bila kuongopa cheo cha mtu”alisema Misime.
Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi
ametoa onyo kwa baadhi ya askari ambao wamekuwa siyo waamni wanaovujisha siri
za Polisi ambazo wananchi wamekuwa wakizitoa kuhusu uharifu na waharifu
Misime alisema, kuwa ili kudhibiti
tabia hiyo askari watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo na kufukuzwa kazi.
Kwa upande wa viongozi wa madhehebu
ya dini wakizungumza baada ya kikao chao
kwisha walisema kuwa watahakikisha wanashirikiana na jeshi hilo,
Kaminyoge Andendekisye ambaye ni
mchungaji wa kanisa la Moroviani Iringa road alisema mahusiano kati ya jeshi la
polisi na upande wao yalikuwa mabovu kutokana na kutotambuliwa kama wana uwezo
wa kuweka hali ya utulivu katika jamii.
Kwa upande wake Usitadhi Musa Jamaa alisema kuwa kitendo
cha jeshi la polisi kukaa nao ni dalili
za jeshi hilo kutambua umuhimu wao hali itakayochagiza kuuweka mjini wa Dodoma
kuwa ni sehemu ya utulifu na amani kutokana na ushirikiano huo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment