Waziri
wa Masahuri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, (kushoto) akiwa na
wajumbe wa amani wa Israel na Palestina siku zilizopita.
Marekani inasema imesikitishwa na makubaliano kati ya makundi makuu Palestina ya kuiunda serikali ya Umoja.
Imeoya huenda hatua hiyo ikatatiza zaidi
jitihada za amani. Uamuzi huo unalijumuisha kundi lenye msimamo kali za
kidini, Hamas, unaliotawala eneo la Gaza na limetajwa na Marekani na
Israeli kama kundi la kigaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Marekani Jen Psaki amesema wakati wa kutangaza uamuzi hduo ndio unaotia wasiwasi.
Tangazo hilo limefanywa wakati ambapo Marekani
ilikuwa ikijitahidi kushawishi Israil na Wapalestina kukubali kuendelea
kufanya mashauriano ya amani ambayo hadi kufikia sasa hayajazaa matunda
yo yote.
Bi Psaki amesema mapatano kati ya Wapalestina
yatavuruga vibaya sana juhudi hizo na akatangaza kuwa itakuwa vigumu kwa
Israil kufanya mashauriano nakundi ambalo haliamini kuwa Israili ina
haki ya kuwepo kama taifa; jinsi wanavyoamini wanachama wa Hamas.
Alisema Serikali ya Marekani itaendelea
kuchunguza kwa makili hatua zinazochukuliwa kuhusiana na uamuzi huo na
Wapalestina siku na hata masaa yanayokuja.
Wamarekani na mataifa washirika wake
wamesisistiza kuwa muda mrefu kuwa taifa lo lote la Wapalastina inapaswa
kuwa lile linaloshutumua vita, litambue Israil na kukubalia mapatano
yote yanayohusisha taifa hilo la Wayahudi.
Wapalestina wanasisitiza kuwa umoja wao utampa
uhalali zaidi Rais Mahmoud Abbas, kufanya mashauriano kwa niaba yao kwa
sababu atakuwa akiwakilisha Wapalestina wote na wala sio baadhi yao tu.
No comments:
Post a Comment