Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro ametimiza umri wa miaka 89 kwa kuandika barua ya wazi kwa taifa lake.
Barua
hiyo ilichapishwa katika gazeti la serikali la Granma ambapo
hajazungumzia lolote kuhusu ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani jijini
Havana utakavyofanya kazi na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John
Kerry.
Badala yake ameituhumu Marekani kwa kuisababishia hasara ya
mamilioni ya dola baada ya miaka mingi ya vikwazo vya biashara baina ya
nchi hizo mbili.
lakini amezungumzia maridhiano ya kihistoria kati ya nchi yake na Marekani.
No comments:
Post a Comment