Wanasayansi
nchini Marekani wamesema kuwa wamefanikiwa kutengeneza chachu yenye
vina saba vinavyoweza kupunguza maumivu kwa kiasi kikubwa.
Chachu
hiyo inaweza kubadilisha sukari kuwa hydrocodone dawa inayofanana na
morphine ndani ya siku tatu mpaka tano. Kwa sasa inachukua mwaka mzima
kuzalisha kundi la dawa za kutuliza maumivu kama hayo kutoka kwenye mmea
aina ya popi.
Hata hivyo, watafiti kutoka chuo cha Stanford
wamesema kazi zaidi inahitajika kwa sababu utafiti wao umeegemea zaidi
kwenye matumizi ya chachu nyingi kutengeneza kidonge kimoja pekee cha
kutuliza maumivu
No comments:
Post a Comment