Polisi na wanajeshi wa Myanmar wamevamia makao makuu ya chama kinachoungwa mkono na jeshi cha Nay-Pyi-daw.
Hakuna
taarifa rasmi iliyotolewa lakini waandishi wa habari katika eneo hilo
wamesema kuwa hali ya sintofahamu katika chama hicho imesababishwa na
ushindani mkali wa kung'ang'ania madaraka katika chama hicho
kinachotawala miezi kadhaa iliyopita.
Na habari zinazotufikia hivi
sasa ni kuwa Spika wa Bunge la Myanmar ameondolewa uwemwenyekiti wa
chama kinachotawala miezi mitatu kabla ya uchaguzi Mkuu.
Mndani wa chama hicho ambaye
hakutaka kujulikana alisema kuwa spika huyo ameondolewa na nafasi yake
kuchukuliwa na mtu asiyependelea mabadiliko ajulikanaye kama Thein Sein.
No comments:
Post a Comment