Wadukuzi wailiza Marekani
Mamlaka
nchini Marekani imewamefungulia mashtaka ya jinai watu tisa baada ya
kuhusika na wizi wa mtandaoni kabla ya kuchapishwa kwa niaba ya
wafanyabiashara wa fedha.
Waendesha mashitaka walisema wadukuzi
hao, walitumia mbinu kutengeneza mamilioni ya dolla ambazo hazikua
halali.Miongoni mwa wanaoshitakiwa ni wadukuzi wa mtandaoni, wafanya
bishara za hisa pamoja na wafanyabiashara wakubwa, ambao Walikua na
matawi yao nchini Ukraine na Marekani.
Kundi hilo la wadukuzi
mtandaoni, linadaiwa kudokoa zaidi ya habari mia moja na hamsini kwa
kipindi cha miaka mitano iliyopita. Mdhibiti wa masuala ya fedha wa
Maekani pia amewafungulia mashtaka watu tisa na watu wengine ishirini na
tatu pamoja na makampuni binafsi yakiwemo pia ya Urusi, Malta, Ufaransa
na Cyprus ambao inasemekana walihusika na udanganyifu.
No comments:
Post a Comment