Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa atangaza baraza jipya la mawaziri

South Africa's deputy President Cyril Ramaphosa at a press conference in London 2017 

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa 

Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo.
Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
Palipotokea anguko la thamani ya randi alilazimika kumfukuza Rooyen na kumchagua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi siku za mbeleni.
Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.
Aliyekuwa mke wake Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma, ameteuliwa kuwa waziri wa ofisi wa rais.
Bw Ramaphosa, ambaye ni mfanya biashara wa umri wa miaka 65, katika hotuba yake ya taifa awali mwezi huu, aliahidi kupambana na rushwa na kuboresha uchumi wa nchi hio.
Aliingia madarkani baada ya mtangulizi wake kuondoka katika hali tete, akikataa shinikizo kubwa ya yeye kujiuzulu.
Utawala wa miaka tisa ya Bw Zuma ulikumbwa na misukosuko ya shutuma za ufisadi wakati nchi ilikuwa ikipambana na madeni ya ndani pamoja na viwango vya juu vya ukosaji ajira.

Kabwe: Tutaendelea kupambana dhidi ya sheria kandamizi Tanzania

Zitto Kabwe,Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo 

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Zitto Kabwe ameachiliwa huru kwa dhamana asubuhi hii baada ya kukamatwa na polisi usiku wa kuamkia Februari 23mkoani Morogoro, karibu kilomita 200 kutoka Dar es salaam.
Sababu ikitajwa ni kufanya mikutano bila kibali alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea viongozi wa chama chao cha ACT Wazalendo maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Alipokamatwa Bw Zitto aliweka ujumbe katika akaunti yake ya Twitter, "Ninasindikizwa hadi kituo cha polisi cha Mgeta wilayani, Mvomero.... Sijaambiwa kwa nini nimekamatwa."
Mbunge Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya shilingi milioni 50 fedha za kitanzania na kudhaminiwa na wakaili wake ndugu Emmanuel Lazarus Mvula.
Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo alikuwa kwenye ziara ya chama chake mkoani humo.
Ametakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi12, 2018.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Zitto Kabwe na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wamesema wataendelea na ziara ya kutembelea kata zinazoongozwa na chama hicho.
Vile vile Zitto akaelezea katika ukurasa wake wa Facebook " Baada ya kulala bure jana polisi Morogoro, tunaendelea na kazi yetu ya kutembelea kata zote ambazo Wananchi walitupa dhamana kwa kuchagua madiwani wa Act Wazalendo."
Katika eneo hilo hilo, taarifa za usiku wa kuamkia leo, zinasema mjumbe mwingine kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA ameuwawa. Taarifa zinasema Diwani huyo wa kata ya Namwawala Godfrey Luena alikutwa nyumbani akiwa mauti baada ya kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

Magufuli na Kenyatta waagiza mawaziri watatue tofauti kati ya Kenya na Tanzania

Kenyatta na Magufuli walipokutana Kampala

 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Tanzania Dkt John Magufuli wamekutana mjini Kampala, Uganda na kuahidi kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Wawili hao wamewaagiza mawaziri wa nchi hizo mbili kutatua tofauti ndogondogo zinazojitokeza katika biashara kati ya nchi hizi mbili.
Marais hao wametoa maagizo hayo walipokutana hoteli ya Munyonyo mjini Kampala muda mfupi kabla ya kuanza kwa vikao vya mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulikuwa umeonekana dorora wiki za karibuni hasa kutokana na hatua ya Tanzania kuwakamata na kuwateketeza vifaranga kutoka Kenya na pia kuwapiga mnada ng'ombe wa watu wa jamii ya Wamaasai kutoka Kenya.
Wawili hao wamesema wanataka kuona biashara kati ya Tanzania na Kenya inazidi kukua na bidhaa zinauzwa na kununuliwa baina ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote na hivyo kuagiza tofauti zilizojitokeza katika baadhi ya bidhaa zimalizwe
Kuna mambo madogomadogo yanakuwa yanajitokeza katika biashara kati ya Kenya na Tanzania, tunataka kwa haya yote Mawaziri wa Kenya na Mawaziri wa Tanzania mkae myatatue, sisi hatuna tatizo, mambo mengine madogomadogo mno, mambo ya viatu, nguo, ngano, gesi ni madogo sana, mnatakiwa myatatue nyinyi yasifike kwetu, sisi huku tuko sawasawa" amesema Dkt Magufuli, tamko ambalo limeungwa mkono na Bw Kenya.
Wametoa maagizo hayo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi upande wa Tanzania.
Upande wa Kenya, maagizo yametolewa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma na Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kaskazini wa Kenya Peter Munya.

Mtangazaji ajifungua akiwa hewani Marekani

Cassiday Proctor, mtangazaji wa kipindi cha redio cha alfajiri katika kituo cha redio cha The Arch katika mji wa St Louis nchini Marekani alitangaza kujifungua kwake kupitia njia ya upasuaji siku ya Jumanne.

Mtangaza mmoja wa redio nchini Marekani amejifungua akiwa hewani wakati wa kipindi chake cha alfajiri.
Cassiday Proctor, mtangazaji wa kipindi cha redio cha alfajiri katika kituo cha redio cha The Arch katika mji wa St Louis nchini Marekani alitangaza kujifungua kwake kupitia njia ya upasuaji siku ya Jumanne.
Bi Proctor alianza kuhisi uchungu wa kujifungua siku ya Jumatatu .Kituo chake cha habari kilishirikiana na hospitali ambayo alijifungua ili matangazo yake kwenda moja kwa moja hewani.
Aliambia BBC kwamba alipata fursa ya kwenda hewani moja kwa moja alipokuwa akijifungua mtoto huyo wiki mbili kabla ya muda uliotarajiwa.
''Ilikuwa furaha kuweza kuwa hewani na wasilikizaji wetu katika siku muhimu ya maisha yangu'' , alisema bi Proctor kuhusu kipindi hicho.
Alisema kuwa kujifungua ukiwa hewani ni mwendelezo ya kile kinachoendelea kila siku katika kipindi hicho ,''mimi huwaambia watazamaji wangu kila kitu kinachoendelea katika maisha yangu.'' .
Mtoto huyo aliyekuwa na uzani wa 7lbs 6oz amepatiwa jina Jameson baada ya wasikilizaji kupendekeza jina la mtoto huyo katika shindano mwezi Januari.
Majina 12 ya kijinga pamoja na mengine 12 yaliochaguliwa na mtangazaji huyo na mumewe yaliwekwa katika sehemu moja .
''Tulipiga kura hadi tulipopata Jameson'', alisema mkurugenzi wa vipindi Scott Roddy .
Mtangazaji mwenza wa bi Proctor Spencer Graves aliambia BBC kwamba hatua hiyo ya kujifungua hewani ilikuwa ya kipekee.
Bi Proctor sasa atakwenda likizo ya uzazi.

Wafanyakazi wa nyumbani waandamana kulalamikia mazingira ya kikazi Kenya

Maadamano ya wafanyakazi wa nyumbani Nairobi 

Wafanyakazi wa nyumbani jijini Nairobi walijumuika na kuandamana wakitoa wito kwa serikali kuwatambua kama wafanyakazi wengine ili pia wao waweze kupata manufaa ya ajira kama vile bima ya afya, likizo ya uzazi na malipo ya uzeeni
Mara nyingi, mfanyakazi wa nyumbani anapokuwa mgonjwa, jambo la kwanza mwajiri anafikiria ni kumfukuza.
Ukizingatia sheria nchini Kenya, wafanyakazi wa nyumbani wana na haki sawa na mfanyakazi mwingine yeyote.
Wanapokuwa wagonjwa, wafanyakazi wa nyumbani wana haki ya kulipwa kikamilifu siku saba za likizo.
Likizo yao ya kila mwaka haipaswi kuwa chini ya siku 21. 

Kisheria, waajiri wanatakiwa kuchangia malipo ya bima ya afya na hazina ya malipo ya uzeeni.
Ruth Khakame, mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Wafanyakazi wa nyumbani anasema kwamba "wafanyakazi wa nyumbani wamekuwa wakifutwa kazi kwa sababu ya ugonjwa, kila siku tunashugulikia kesi za aina hii".

Kwa mujibu wa shirika la Kituo Cha Sheria, wafanyakazi wa nyumbani ni miongoni mwa makundi yanayokumbwa na changamoto zaidi.
Muungano wa wafanyakazi wa nyumbani, ambao umesajili zaidi ya wafanyakazi wa nyumbani 16,000, umekuwa ukiandaa vikao mara kwa mara kusikiliza malalamishi na kuwahamasisha wanachama.
Beatrice Atieno, amefanya kazi hii kwa miaka 15 na huwa anahudhuria vikao hivi "unaweza kupata kuwa unafanyia mtu kazi kwa nyumba yake na hakuheshimu, hakuamini, ikifika wakati wa chakula anakubagua, anakupatia chakula kidogo, huwezi kushiba, na wewe ndio unamtunza mtoto wake, na wewe ndio unachunga nyumba yake".
Kwa mujibu wa Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) asilimia 30 ya wafanyakazi wa nyumbani huwa ni watoto. Wanawake wanajumuisha asilimia kubwa.
Kenya peke yake, wafanyakazi wa nyumbani ni zaidi ya milioni 2.

 

Mwanamume atolewa uvimbe wa kilo 1.8 kwenye ubongo India

Mr Pal's brain tumour was larger than his head 

Madaktari nchini India wamefanya upasuaji wa kipekee na kuondoa uvumbe wa uzani wa kilo 1.8 kutoka kwa mwanamume wa umri wa miaka 31.
Wanasema huo huenda ukawa uvimbe mkubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye ubongo wa binadamu.
Upasuaji huo, ambao ulidumu saa saba, ulifanyika mnamo 14 Februari katika hospitali ya Nair mjini Mumbai magharibi mwa nchi hiyo.
Lakini taarifa za upasuaji huo hazikutangazwa moja kwa moja kwa sababu madaktari hawakuwa na uhakika iwapo ulifanikiwa.
"Sasa ni suala tu lake kupona, lakini maisha yake hayamo hatarini tena," Dkt Trimurti Nadkarni, mkuu wa upasuaji wa mfumo wa neva, ameambia BBC.
Santlal Pal, mwuzaji duka kutoka jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, amekuwa akiishi na uvimbe huo kwa miaka mitatu.
Madaktari wanasema Pal alipoteza uwezo wake wa kuona kutokana na uvimbe huo.
Hata hivyo, kuna matum
Mke wake ameambia gazeti moja India kwamba alikuwa ameambiwa na madaktari katika hospitali tatu tofauti Uttar Pradesh kwamba uvimbe huo hauwezo kuondolewa.
"Visa kama hivyo huwa hatari sana," Dkt Nadkarni alisema, na kuongeza kwamba Pal alihitaji painti 11 za damu wakati wa upasuaji huo.
Aidha, alitumia mtambo wa kumsaidia kupumua kwa siku kadha baada ya upasuaji huo.
aini kwamba huenda akapata uwezo wa kuona tena baada ya kupona.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule kama lile lililowaua watu 17 wiki iliopita mjini Florida.

Baada ya mauaji ya watu 17 katika shule moja Florida 14 Februari, na mwaka jana kufuatia kuuawa kwa watu 59 jijini Las Vegas, Nevada watetezi wa udhibiti wa silaha nchini Marekani wameanza kuzidisha kampeni yao.
Ni kisa ambacho kinaonekana kuwa cha kawaida, kwani hilo hutokea kila baada ya mauaji kutekelezwa kwa kutumia bunduki.
Katika ngazi ya taifa, licha ya utafiti kuonyesha kwamba watu wengi wangependa kukazwa kwa sheria za kuwaruhusu watu kumiliki silaha, bado hakuna hatua iliyochukuliwa kutunga sheria kwa miongo kadha.
Miongoni mwa mambo ambayo hupendekezwa ni uchunguzi zaidi wa historia na maisha ya mtu kabla yake kuuziwa silaha.
Aidha, kupigwa marufuku kwa bunduki zenye uwezo mkubwa sawa na zile zinazotumiwa na jeshi.
Baada ya idadi kubwa ya watu kuuawa wakati huu, huenda shinikizo za kufanyika kwa mabadiliko zitazidi.
Hapa chini ni sababu nne ambazo zimezuia kufanyiwa mageuzi kwa sheria kuhusu silaha Marekani.