Ajali Asubuhi Yatokea Asubuhi Hii Dar

Mmoja wa wanadada (mwenye suti) waliokuwamo ndani ya gari akifarijiwa. Mwenzake alikimbizwa Marie Stopes kwa kwa huduma ya kwanza

Na: Rodrick Maro

Japo inasemekana kuwa ajali haina kinga, ila tahadhari ni muhimu. Barabara inayounganisha Shekilango na Alli Hassan Mwinyi, eneo la Sayansi, lipo katika matengenezo.

Hivyo, inapaswa madereva kuchukua tahadhari, kwani barabara hiyo haijakamilika na pia mkandarasi yupo kazini.Bahati mbaya sana, asubuhi hii, majira ya saa Moja, wanadada wawili wamejikuta gari lao, Escudo likigeuka lilikotoka na kuwa miguu juu, mbele kabisa la Jengo la Kituo cha Sheria na Haki za Biandamu (Justice Lugakingira House)! Ila la kumshukuru MUNGU ni kuwa wamepona, japo hawakuepuka michubuko midogo midogo.


Rodrick Maro

LHRC,

P. O. Box 75254,

Dar es Salaam.

Phone: +255 22 2773038/48

Fax: +255 22 2773037 Mob: 0713 51 92 18

No comments:

Post a Comment