AIRTEL TANZANIA NA PUMA ZACHANGIA KUFANIKISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI



Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mh, Pereira Ame Silima akipokea sehemu ya ya stika maaalum kwa ajili ya kampeni ya Usalama barabarani toka kwa wadhamini wa stika hizo kwa mwaka huu Airtel na Puma, wnaokabidhi toka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa airtel Bi Beatrice Singano na Mkurugenzi wa kampuni ya Mafuta Puma bw, Maregesi Manyama. Anaeshudia makabidhiano ni kamanda mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi Mpinga. Airtel Tanzania na Puma ni wadhamini wakuu wa wiki ya uhameasisaji wa wiki ya Nenda kwa usalama ambapo mwaka huu kitaifa itafanyika mkoani iringa ikiwa imebeba ujumbe usemao “ Pambana na ajiali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria



Kamanda mkuu kikosi cha usalama barabarani Mohamedi Mpinga akionyesha (WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI) jinsi ya kufungua na kubandika stika maaalum kwaajili ya kampeni ya kudhibiti Usalama barabarani mara baada ya kukabidhiwa stika hizo na wadhamini wao kampuni ya simu za mkononi Airtel na Puma, wanashudia pichani toka kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa airtel Bi Beatrice Singano na Mkurugenzi wa kampuni ya Mafuta Puma bw, Maregesi Manyama, na kushoto ni Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mh, Pereira Ame Silima, wiki ya Nenda kwa usalama mwaka huu kitaifa itafanyika mkoani iringa ikiwa imebeba ujumbe usemao “ Pambana na ajiali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria

No comments:

Post a Comment