Nilichokisia Kwenye Mkutano Wa CUF Jangwani



 baadhi ya magazeti ya jana

Juzi Chama Cha CUF Kilifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.nilikuwepo binafsi nikichukua picha na kusikiliza hotuba mbalimbali.pamoja na mambo mengine,CUF Inaonekana kutokuwasema vizuri wana habari.na nilisikia mwenyewe kutoka hotuba za viongozi,isipokuwa Lipumba pekee mashambulizi,ama vijembe kwa wanahabari.Viongozi wa CUF wanaamini vyombo vya habari havipendi,ama vinapotosha,ama vinabeza habari kuhusu chama chao,na nilisikia watu wa kawaida wakiazimia kupiga waandishi watakaohudhuria mkutano wao baadaye ikiwa ule wa jangwani hautaonekana kupewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari,hususani magazeti.Na kweli nimefuatilia magazeti ya jana,mengi hayakutoa uzito wowote kwa habari ya CUF.Mtanzania waliweka picha ya umati,lakini habari yao kuu ilihusu taarifa ya awali ya mkutano wa kamati kuu ya CHADEMA,hicyo hivyo magazeti mengine.

 Sasa ni kweli upo mgogoro kati ya waandishi na CUF?,kama ndiyo,umesababishwa na nini,na kama hakuna ugomvi,nini kinapelekea habari za CUF kutopata uzito unaostahili kwenye vyombo vya habari? je yawezekana ni mikakati ya washindani wao kisiasa yaani CCM na CHADEMA kwamba CUF wasipewe uzito? na ama ni udhaifu wa idara ya habari ya chama cha CUF yenyewe kutotenda kazi ipasavyo? maana nikiri pia kuwa japo mimi ni mwanahabari sikumjua afisa habari wa CUF hadi juzi alipotambulishwa mkutanoni. Na katika mengi ama yawezekana hii ni kutokana na CUF kushuka umaarufu kisiasa kiasi kwamba habari zake hazivuti wasomaji? naomba mitazamo yenu.

Msaidizi wa Mwenyekiti,Dar

No comments:

Post a Comment