Usafiri Wa Treni Waanza Kwa Majaribio
Usafiri
wa treni jijini Dar es saklaam utaanza mwezi Oktoba baada ya kukamilika
kwa maboresho ya reli kutoka Ubungo hadi stesheni.
Akizungumza
jana baada ya kufanya safari ya majaribio Naibu waziri wa Dk Charles
Tizeba alisema kufikia mwezi ujao treni hyo ityaanza kubeba abiria ili
kupunguza matatizo ya usafiri kwa wakazi waishio maeneo inapopita treni
hiyo.
“Kufika
Oktoba tutakuwa tumeanza kutoa huduma maana leo tumeanagalia uwezekano
na tumeona tunaweza ufanya huduma na kurekebisha kasoro zilizobaki”
alisema Dk Tizeba .
Dk
Tizeba alisema kuwa reli hiyo kwa sasa bado haijakaa vizuri hivyo
inahitaji kurekebishw aili trenio hiyo iwee kwenda kasi zaidi na
kubomolewa kw anyumba zilizojengwa jirani na reli hiyo.
“Inashangaza
sana kwani kuna watu wamejenga nyumba zao jirani kabisa na reli na
wengine wamediliki kujenga mita moja kutoka relini, hii inahatarisha
maisha yao wengyewe na hata wasafiri watakaotumia ttreni”
Hivyo
alisema kuwa tayari watu hao wametaarifiwa juu ya kuondoka katika
maeneo hayo na kwamba watatakiwa kuvunja wenyewe na wakikaidi basi
watavunjiwa ili huduma hiyo ianze kutolewa.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment