Idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa homa ya Ebola, katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefika watu 31 hadi kufikia sasa na hata inatishia kuathiri miji kadhaa.
Hili ndilo onyo limetolewa na shirika la afya duniani WHO.
Mipuko wa kwanza wa homa hiyo uliripotiwa tarehe kumi na saba mwezi wa saba katika mkoa wa Kaskazini Mashariki wa Orientale.
Afisaa mmoja wa shirika hilo Eugene Kabambi aliambia shirika la habari la Reuters kuwa hali ni mbaya sana na kwamba bado haijadhibitiwa.
Ni rahisi sana kuambukizana homa ya Ebola na homa hiyo huuwa asilimia tisini ya watu ambao huambukizwa.
Hakuna tiba inayojulikana kwa homa hiyo wala chanjo. Homa hiyo husambaa kwa kugusana na husababisha mgonjwa kuvuja sana damu.
Idadi ya vifo vilivyotokana na homa yenyewe katika miji ya Isoro na Viadana, imeongezeka maradufu kwa zaidi ya wiki moja hadi watu 31.
Homa ya Ebola
No comments:
Post a Comment