Mwandishi Afukuzwa Uanachama Baada Ya Kuwasaliti Wenzake
MUSOMA
CHAMA
cha Waandishi wa Habari mkoani Mara MRPC, kimemfukuza uanachama wa
chama hicho, mwandishi wa habari wa radio Free Afrika mkoani Mara Bw
Maxmilian Ngesi baada ya kukiuka makubalino ya chama hicho yaliyofikiwa
juzi ya kutoandika kabisa habari za jeshi la polisi mkoani humo.
Akizungumzia
kufukuzwa kwa Mwandishi huyo mwenyekiti wa chama hicho Bw Emmanuel
Bwimbo,alisema kuwa Ngesi amekiuka makubaliano ya waandishi wenzake na
chama kwa ujumla baada ya kusikika akitangaza habari za jeshi la polisi
kwa kumkariri kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara.
“
Sisi kwa kauli moja tumekubaliana kutofanya kazi na Jeshi la Polisi
Mkoani Mara baada ya Matukio kadhaa likiwemo ya kuuawa kwa mwandishi wa
habari mkoani Iringa na kutunyima kibali cha Maandamano yetu ya Amani
kupinga Mauaji hayo” alisema Bw Bwimbo
Bw
Bwimbo alisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani mwandishi huyo
alivyokiuka makubaliano ya pamoja na kuwasaliti wenzake ambao
wamekubaliana kwa pamoja kuwa hawataandika habari za jeshi hilo kutokana
na kuzuiwa waandishi kutoandamana katika maandamano ambayo yaliitishwa
nchini kote kulaani kitendo cha mauaji ya mwandishi wa kituo cha chanel
Ten mkoani Iringa Daud Mwangosi.
Alisema
Ngesi kama mwanachama alitakiwa kutii maamuzi ya chama na tamko la
chama chake kwa vile tamko hilo limewataka wananchama wote na siyo kwa
mkoa wa Mara tu lakini pia baadhi ya mikoa imetoa matamko na misimamo
hiyo lakini cha kushangaza yeye amekaidi na kwenda kinyume.
Aidha
Mwenyekiti huyo alisema kamwe chama hicho hakiwezi kuvumilia mwandishi
atakaye kiuka agizo hilo na hatua ambayo imechukuliwa kwa Ngesi ni mfano
kwa waandishi wengine hadi hapo tamko hilo litakapo tenguliwa.
Jumatatu
wiki hii waandishi wa habari walifanya maandamano nchi nzima wakilaani
mauaji ya mwandishi mwenzao Daudi Mwangosi ambapo kwa mkoa wa Mara
maandamano hayo yaliuzuiwa na polisi hali iliyofanya chama cha waandishi
wa habari kukataa kuandika habari za jeshi hilo mkoani Mara.
No comments:
Post a Comment