Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari- Ligi Kuu Ya Vodacom Tanzania Bara Kuanza Kesho
Release No. 145
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 14, 2012
VPL 2012/2013 KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO
Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara 2012/2013
inaanza kutimua vumbi kesho (Septemba 15 mwaka huu) ambapo timu zote 14
zitakuwa kwenye viwanja saba tofauti.
Mabingwa
watetezi Simba wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam. Mjini Morogoro, Polisi Dodoma watakuwa wenyeji wa Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati jijini Tanga, Mgambo JKT ambayo
imepanda daraja msimu huu itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa
Mkwakwani.
Tanzania
Prisons ambayo nayo imerejea VPL msimu huu itaialika Yanga kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. JKT Ruvu na Ruvu Shooting
zitapambana kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam huku Azam
ikiwatembelea Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba.
Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto
Africans dhidi ya Oljoro JKT. Mechi zote zitaanza saa 10.30 jioni.
Viingilio
katika mechi ya Simba na African Lyon vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya
rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000
viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Viingilio kwa
mechi nyingine vitakuwa sh. 3,000 na sh. 10,000.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment