Zimbabwe inamsaka mshukiwa wa Rwanda
Polisi nchini Zimbabwe, wanasema kuwa
wameanzisha msako mkali wa afisaa mmoja mkuu wa zamani nchini Rwanda
ambaye anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya Kimbari mwaka 1994 nchini
Rwanda.
Protais Mpiranya alikuwa kamanda wa ulinzi wa
rais mwaka huo na anatuhumiwa kwa kuhusika pakubwa na mauaji ya watutsi
800,000 pamoja na wahutu wenye msimamo wa kadri.
Zimbabwe imekuwa ikishutumiwa kwa kumpa hifadhi afisaa huyo wa zamani.
Makama maalum kuhusu mauaji wa kimbari nchini
Rwanda imeahidi kumkabidhi zawadi ya dola milioni tano yeyote mwenye
taarifa kumhusu Protais.
"Tunamtaka. Awe hai au akiwa amekufa. Tunatafuta
taarifa kumhusu ili tumkamate.Hatufahamu mda ambao amekuwa akiishi hapa
nchini'' alisema afisaa mkuu wa polisi Zimbabwe Peter Magwenzi.
Mwaka jana afisaa mmoja wa nchi hiyo alikana kuwa Zimbabwe inamhifadhi Protais.
No comments:
Post a Comment