Bomu lauwa waumini 7 Kaduna, Nigeria
Takriban watu saba wameuawa
nchini Nigeria na wengine wengi wakijeruhiwa katika shambulio la kujitoa
mhanga katika kanisa la kikatoliki Kaskazini mwa Nigeria.
Maafisa wanasema kuwa gari lililokuwa limebeba
mabomu liliingia katika kanisa hilo na kulipua mabomu huku athari zake
zikitoboa shimo katika paa la kanisa hilo.
Shambulio hilo lilitokea mjini
Kaduna, eneo ambalo limekuwa likilengwa sana na wapiganaji wa Boko Haram
kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni.
Rais Goodluck Jonathan ameahidi kongeza juhudi
za kupambana na ugaidi na vurugu nchini humo. Aidha Rais Goodluck
alitaja shambulizi hilo kama kitu kisicho kubalika na ambacho kinatishia
usalama na uthabiti wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC mjini huko anaarifu kuwa
shambulio hilo lilitokana na bomu lilotegwa kwenye gari lililopuliwa na
mtu aliyejitoa mhanga na kugonga gari hilo kwenye ukuta wa kanisa.
Anasema uharibifu mkubwa ulitokea ndani ya jengo na kwamba mapaa ya maduka na nyumba za karibu yaling'oka.
Afisaa wa kanisa alisema watu kama wanne waliuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Wakuu wanasema vijana wa Kikristo walioingiwa na
hasira kwa sababu ya tukio hilo, walishambulia gari la serikali ambalo
lilikwenda kusaidia manusura.
Kumetokea mashambulio kadha ya kidini katika jimbo hilo, mengi yamefanywa na kundi la wapiganaji wa kiislamu, Boko Haram.
No comments:
Post a Comment