Mbinu mpya ya bei nafuu kupima HIV
Ikiwa mtu anavirusi rangu ya kifaa inabadilika kuwa buluu na ikiwa hana rangi unakuwa nyekundu
Aina mpya mbinu
ya kuchunguza na kuona hata viwango vya chini vya virusi na hata aina ya
saratani imezinduliwa na watafiti nchini Uingereza.
Utafiti huo unahusu majimaji ambayo hubadilika rangi kuonyesha ikiwa mtu ameathirika au la.
Watafiti wa uchunguzi huo kutoka
chuo kimoja kikuu mjini London wanasema kuwa mbinu hiyo inaweza
kuchangia kuhamasisha watu kupimwa Virusi vya HIV na magonjwa mengine
ambako njia zengine za kupima maradhi ni ghali
Aidha watafiti wansema mbinu hii mpya ambayo
inahitaji utafiti zaidi, inaweza kuelezea kwa kina aina ya ugonjwa au
virusi mfano proteni inayopatikana kwenye kirusi cha HIV.
Ikiwa dalili ya kirusi au ugonjwa ipo katika
matokeo ya uchunguzi, basi inabadili rangi ya kemikali. Matokeo
yatakuwa rangi ya buluu ikiwa kirusi kipo na nyekundu ikiwa kirusi au
ugonjwa haupo.
Watafiti wanasema kuwa matokeo ya uchunguzu au upimaji pia yatapatikana mara moja.
Profesa Molly Stevens aliambia BBC: " Mbinu hii
ya kupima magonjwa inatumiwa kuchunguzwa virusi hata kama ni vya viwango
vya chini mno na kuongeza nafasi ya kuona ikiwa ugonjwa upo kwenye
mwili wa mtu au la.
Hiki ni kifaa ambacho mtu anaweza kujipima mwenyewe hali yake ya HIV akiwa nyumbani
"Kwa mfano, ni muhimu kuchunguza viini vya
ugonjwa vilivyo na viwango vya chini sana vya mfano saratani kwa mtu
aliwahi kutibiwa ugonjwa huo kuona ikiwa saratani hiyo itaweza kuibuka
tena hata baada ya kutibiwa."
"pia inaweza kusaidia katika kupima wagonjwa wa
HIV, ambao viwango vya virusi viko chini sana kiasi cha kutoweza
kuonekana kwa mbinu za sasa."
Watu waliopimwa mapema kutumia mbinu hii ya
rangi, walionyesha dalili za HIV na saratani ya tezi ya kibofu, ingawa
utafiti wake katika nyanja za juu bado utahitajika kabla ya kutumika
hospitalini.
Watafiti wanasema kuwa wanatarajia kuwa gharama
ya kifaa hicho itakuwa ndogo mara kumi kuliko mbinu za sasa za kupima
magonjwa na kwamba itanufaisha watu katika nchi ambazo mbinu zilizopo
hawawezi kuzimudu. Na pia itaweza kutumika sana katika kupima virusi vya
HIV katika nchi maskini duniani.
No comments:
Post a Comment