Marekani yatahadharishwa kuhusu 'Sandy'
Kimbunga Sandy
Rais wa
Marekani Barack Obama, amewatahadharisha wamarekani kuchukulia kwa uzito
kimbunga Sandy huku maafisa wakianza kufunga eneo la Mashariki mwa
pwani ya nchi hiyo wakisubiri kimbunga hicho kupiga.
Majimbo kadhaa yametangaza hali ya hatari huku
mamilioni ya watu wakiathiriwa na dhoruba kali wakati shule na barabara
zikifungwa.
Wataalamu wanahofia kimbunga hicho huenda kikawa kikali mno wakati kitakapopiga sehemu za nchi hiyo.
Baadhi ya mikutano ya kisiasa ya hadhara
imesitishwa huku Rais Obama akionya watu kuchukua hatua za kujikinga na
athari za zaidi za kimbunga hicho.
Usafiri wa kimataifa kutoka nchini humo
umeathirika sana. Mashirika ya ndege ya Ufaransa, Uingereza na Virgin
Atlantic yamesitisha safari zao katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo
ikiwemo miji ya , New York, Baltimore, Newark, Washington, Boston na
Philadelphia kuanzia leo.
Kwa mujibu wa idara ya utabiri wa vimbunga, saa
nane asubuhi ya leo, kimbunga hicho, kilianza kuelekea Kaskazini
kikienda kwa kasi ya kilomita 760, Kusini Mashariki mwa mji wa New York.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika miji ya Maryland, New York, Pennsylvania, Virginia, Washington DC na North Carolina.
Kimbunga hiki kinatoa fursa kwa Rais Obama
kuonyesha uongozi wake mbali na siasa na ikiwa atakosa kuonyesha uongozi
unaostahili huenda wakosoaji wake wakatumia fursa hiyo kumponda na
kumlaumu kwa kosa lolote.
No comments:
Post a Comment