Kesi ambayo bingwa wa Olimpiki
wa Kenya, Ezekiel Kemboi alishtakiwa kwa kumshambulia Ann Njeri Otieno
mjini Eldoret Mkoani Rift Valley mwezi wa Julai mwaka huu, imetupiliwa
mbali na mahakama mjini humo
Kulingana na hakimu wa mahakama ya Eldoret Francis Kyambia mlalamishi Njeri amekubali kesi hiyo waimalize nje ya korti.
Anne Njeri Otieno alidai kuwa
mwanaridaha huyo alimshambulia alipokataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi
naye mwishoni mwa mwezi Juni .
Lakini kabla ya kesi hiyo kusikilizwa tena, Bi Njeri Otieno aliambia mahakama kuwa alimua kumwodolea mashtaka Kemboi.
Bwana Kemboi, anayefanya kazi katika idara ya polisi daima amekuwa akikanusha madai hayo
Hakimu alimwachilia kwa dhahama ya dola 230
mwanariadha huyo mwishomi mwa mwezi Juni na kumruhusu ashiriki michezo
ya Olimpiki mjini London ambako alishinda medali yake ya pili ya
dhahabu.
Ann Njeri Otieno
Bi Njeri aliwaambia waandishi wa habari kuwa alifutilia mbali kesi hiyo kwa sababu anataka kuendelea na maisha yake.
Njeri alikuwa amemshtaki Kemboi kwa kumshambulia
na kisu nje ya nyumba yao iliyoko mtaa wa West Indies mjini Eldoret
akiwa ndani ya gari lake. Lakini Kemboi alidai ni Njeri ndiye
aliyemshambulia akiwa na watu wanne.
Hatimaye Kemboi, ambaye hufurahisha mashabiki
sana kwa densi yake murwa kila anapoibuka mshindi uwanjani, alisafiri
hadi London na timu ya Kenya na kushinda dhahabu mbio za mita elfu tatu
kuruka viunzi na maji.
No comments:
Post a Comment