Jeshi la Sudan limesema watato
wawili wameuawa kufuatia mashambulio mapya ya mabomu yaliyotekelezwa na
waasi katika mji mkuu wa jimbo la Kordofan ya Kusini.
Msemaji wa jeshi la nchini hiyo amesema kuwa raia wanane walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo mjini Kadugli.
Kundi la waasi wa SPLM-North nchini Sudan
limesema lilikuwa likijibu mashambulio ya siku kadhaa yaliyotekelezwa
dhidi yao na wanajeshi wa serikali
Umoja wa mataifa unakadiria kuwa maelfu ya watu
wamehama makwao na wengine wengi kuathirika kutokana na mapigano hayo
katika eneo la Kordofan ya Kusini, tangu uasi huo ulipoanza mwaka
uliopita wakati Sudan Kusini ilijapatia uhuru wake.
No comments:
Post a Comment