Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki amesema ujenzi wa kituo kipya cha mabasi
yaendayo mikoani kinatarajiwa kujengwa eneo la Mbezi Ruis.
Akizungumza na NIPASHE, alisema serikali imeanza mkakati wa kuwahamisha
wakazi wa eneo hilo ili kupisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi kwani
kituo cha Ubungo kinachotumika hivi sasa, kitatumika kwa ajili ya mabasi
yaendayo kwa kasi (DART).
Alisema kwa mabasi yanayofanya safari zake ukanda wa Kaskazini
yatajengewa kituo eneo la Boko na eneo la machimbo lililopo Kunduchi
jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wao Chama Cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), baada ya kutishia
kutohama katika Kituo cha Ubungo na kuunda tume ya watu watano ili
kufikisha malalamiko yao kwa Mkuu wa mkoa wamesema kuwa wamekubaliana na
uamuzi huo wa Serikali baada ya kushirikishwa kuhusu ujenzi huo.
Aidha, Katibu wa chama hicho, Enea Mrutu, alisema baada ya kukutana na
Mkuu wa Mkoa na kufafanuliwa juu ya suala hilo, chama kimeridhia ujenzi
huo na hakutatokea vitisho vingine kuhusu kugoma kuhama Ubungo.
Hata hivyo, Mrutu alisema pamoja na kituo kipya kujengwa eneo husika,
bado kutakuwepo na usumbufu mkubwa kwa wasafiri hasa wale waishio mbali
na kituo hicho.
No comments:
Post a Comment