Makabiliano
makali yamezuka kati ya Polisi na wachimba migodi katika mgodi wa madini
ya Platinum wanaogoma Kaskazini Magharibi mwa Johannesburg.
Polisi waliwafyatulia risasi za mipira na
kuwarushia waandamanaji gesi ya kutoa machozi katika makabiliano hayo
ambapo wachimba madini hao wanataka nyongeza ya mishahara.
Kampuni ya Anglo-American Platinum imekubali
kuwarudisha kazini wachimba madini elfu kumi na mbili waliofutwa kazi na
kuwalipa malimbikizo ya mishahara, suala lililokataliwa mbali na
wachimba madini hao.
Msururu wa migomo ya wachimba migodi na madini
imeendelea kukumba Afrika Kusini katika miezi ya hivi karibuni na
kuathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment