Washukiwa wa mauaji wakamatwa Nigeria
Polisi katika eneo la kaskazini
mwa Nigeria wamesema wamewatia nguvuni washukiwa kadha kuhusiana na
mauaji ya takriban watu 26 katika bweni la wanafunzi mjini Mubi.
Maafisa wa Serikali wanasema inaonekana waliouawa ni watu waliojulikana na kulengwa na wavamizi waliowatambua kwa majina.
Hapo awali ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji la, Boko Haram, lilihusika.
Hata hivyo, kiongozi mmoja wa zamani wa
mwanafunzi ameiambia BBC kwamba huenda mauaji hayo yalichochewa na
uhasama kati ya makundi ya wanafunzi yaliyoshiriki kwenye uchaguzi
uliofanyika katika chuo kimoja cha mafunzo katika eneo hilo.
Ken Henshaw, aliyekuwa Rais wa Chama cha kitaifa
cha Wanafunzi nchini Nigeria, amesema hakujawahi kufanyika uchaguzi wa
wanafunzi bila kuwepo kwa umwagikaji wa damu tangu mwaka 2002.
Aliongezea kusema kwamba uchaguzi huo
huchukuliwa kuwa ngazi ya kuelekea kwenye nyadhifa kuu za kisiasa
Serikalini katika siku za uson
No comments:
Post a Comment