WATUHUMIWA UCHOMAJI WA MAKANISA MBAGALA, WAPANDISHWA TENA KIZIMBANI
Na Musa Mateja
WATUHUMIWA 47 wanaokabiliwa na kesi ya kuharibu na kuchoma moto
makanisa wakati wa vurugu za baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu
Mbagala, leo wamepandishwa tena kizimbani katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka mbele ya Wakili Mwandamizi wa
Serikali, Bw. Tumaini Kweka, yanayowahusisha na kesi ya kula njama kwa
nia ya kutenda makosa kinyume na sheria.
Askari magereza akiwafungulia pingu baadhi ya watuhumiwa tayari kwa kusomewa mashitaka yao.
Makosa mengine yanayowakabiri watuhumiwa
hao ni pamoja na kosa la kuvunja jengo kwa nia ya kufanya uharifu,
uharibifu wa mali za kanisa, wizi wa vifaa vya kanisa, kuchoma kwa
makusudi jengo linalotumika kwa shughuli za ibada na kuhatarisha maisha
ya mlinzi. Mashitaka yote hayo leo yamewakilishwa mbele ya Hakimu,
Bw. Binge Mashabala, ambaye alisikiliza pande zote mbili na kuahirisha
kesi hiyo hadi Novemba 7 mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha upelelezi wa
kesi hizo.
Watuhumiwa wakipelekwa kizimbani.
…wakipanda ngazi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama.
Baadhi ya watuhumiwa 47 waliyofikishwa kizimbani wakiwa ndani ya mahakama.
Wakirejeshwa mahabusu.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa watuhumiwa hao wakiwa nje ya mahakama. (Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
No comments:
Post a Comment