Bunge la Congress la Libya limeidhinisha baraza jipya la mawaziri linaloongozwa na waziri mkuu Ali Zidan.
Kura hiyo inakuja siku moja baada ya
waandamanaji ambao hawakufurahia muundo wa baraza hilo kutatiza mkutano
wa kuidhinisha bunge hilo.
Orodha ya Bwana Zidan inajumuisha
mchanganyiko wa mawaziri wasio na siasa kali na wale wenye siasa kali
wakati akijaribu kuunda serikali ya muungano, itakayoridhisha kila chama
Waziri mkuu aliyetangulia ,Mustafa Abu Shagur, aliachishwa kazi baada ya Congress kufutilia mbali baraza lake la mawaziri
Ni thuluthi mbili tu ya wabunge wa bunge hilo
lenye wanachama 200, walihudhuria kikao hicho siku ya jumatano , kikao
kilikamilika punde baada ya maombi.
Mkuu wa Congress Mohammed Magarief, alisema kuwa alishauriwa na walinzi wake akamilishe vikao vyake mapema.
Takriban watu 100 walisimama nje ya bunge ingawa hapakuwa na vurugu mfano ya zilizotokea siku ya jumanne.
Baraza la pamoja
Serikali mpya ina waakilishi kutoka vyama viwili
vikubwa vya bunge la Congress , chama cha ‘Alliance of National Forces’
kinachoongozwa na waziri mkuu wa zamani mliberali, Mahmoud Jibril, na
chama cha Muslim Brotherhood pamoja na kile cha Construction Party.
Kulingana na orodha hii, wizara za ulinzi na
usalama wa ndani, zitaongozwa na mawaziri kutoka mji wa Mashariki mwa
Benghazi ambao unaonekana kuwa kitovu cha mapinduzi ya mwaka jana dhidi
ya serikali ya hayati Muammar Gaddafi.
Wanawake wawili ni miongoni mwa wale walioteuliwa kwenye baraza hilo naye bwana Zidan.
Waandamanaji mnamo siku ya jumanne walisema kuwa baadhi ya mawaziri waliopendekezwa walikuwa na uhusiano na kanali Gaddafi.
Licha ya uchaguzi wa amani kufanyika mwezi
Julai, kipindi cha mpito kingali kinaendelea nchini Libya licha ya
kukumbwa na msukosuko
No comments:
Post a Comment