
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee amewasilisha hoja binafsi
bungeni akiitaka Serikali kusitisha ugawaji wa ardhi hadi tathmini
ifanyike, huku akimtuhumu Waziri Mkuu kuwa anashiriki katika
kuwakumbatia wawekezaji wanaopora ardhi wananchi.
Mdee amesema kuwa bila kufanya hivyo, ardhi yote ya nchi hii itachukuliwa na wawekezaji huku wananchi wakiachwa masikini.
Akiwasilisha
bungeni hoja binafsi kuhusu kusitishwa ugawaji ardhi nchini, Mdee
aliitaka Serikali kusitisha ugawaji wa ardhi hadi hapo tathmini ya kina
itakapofanyika kujua kiasi cha ardhi kilichopo mikononi mwa wawekezaji.
Vile
vile, alitaka tathmini ya kina ifanyike kubaini raia wa kigeni na wa
ndani waliojipatia ardhi kinyemela kupitia Serikali za vijiji kinyume na
matakwa ya sheria ya ardhi namba 5 ya mwaka 1999.
“Kwa mujibu wa
Kanuni namba 54(1), (2) na (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo
la 2007 naomba kutoa hoja binafsi ya kuitaka Serikali kusitisha ugawaji
wa ardhi kwa wawekezaji wa ndani na wa nje mpaka hapo tathmini ya kina
itakapofanyika kubaini ni kiwango gani cha ardhi kiko mikononi mwa
wawekezaji,” alisema Mdee.
Alisema katika miaka ya hivi karibuni,
kutokana mtikisiko wa uchumi duniani, tumeshuhudia wimbi la wawekezaji
kutoka nje wakingia nchini kuwekeza katika kilimo kwa maelezo kwamba
watasaidia kuinua uzalishaji katika sekta ya kilimo.
Hata hivyo, alisema uwekezaji huo wa wageni katika ardhi umegeuka kuwa shubiri kwa wananchi hususan wakulima wadogo.
Alisema
wakulima hao wamekuwa wakiondolewa katika maeneo yao ya asili ili
kuwapisha wageni huku wakiachwa katika lindi la umasikini mkubwa.
Mdee alisema ardhi hiyo imekuwa ikichukuliwa na Serikali kuwa haina mwenyewe au haitumiki.
“Hii
inatokana na ukweli kwamba kumekuwa na tafsiri ambayo sio sahihi,
kwamba ardhi wanayopewa wawekezaji haina wenyewe, haina mtu, haitumiki.
Wakati ukweli ni kwamba maeneo mengi kama sio yote yalikuwa yanatumiwa
na wakulima wadogo,” alisema.
Mdee alisema wawekezaji wamechukua
maeneo makubwa ambayo wameshindwa kuyaendeleza na hata yale ambayo
wanayaendeleza ni kwa kiasi kidogo.
Alisema baadhi ya waewekezaji
wengine baada ya kumilikishwa ardhi kwa bei ya kutupa wamekuwa wakikaa
nayo na baadaye kuiza kwa wawekezaji wengine.
Mdee aliliomba Bunge kukubali Serikali kusitisha ugawaji wa ardhi ili kuangalia wapi ilipokosea kwa manufaa ya nchi.
Mbunge
huyo kupitia Chadema, alisema hata wizara ya ardhi na maendeleo ya
makazi wakitakiwa leo kutoa taarifa sahihi ya ardhi kiasi gani iko chini
ya miliki ya wageni hawana taarifa hizo.
Alisema kutokana na
waewekezaji kupewa ardhi bila ya kufuata taratibu, hivi sasa migogoro
mingi ya ardhi iliyopo nchini inatokana na wananchi kuporwa ardhi kwa
kisingizio cha uwekezaji.
Alitoa mfano wa Kampuni ya Kigoma
inayofahamika kama Agrisol na FELISA ambayo imenunua hekari 3,000 katika
Kijiji cha Basanza Kata ya Uvinza wilayani ya Uvinza.
Alisema wawekezaji hao ambao wanakingiwa kifua na Waziri Mkuu, wamewakuta wakulima na wafugaji katika maeneo haya.
Alisema
mwekezaji kwa kushirikiana na vyombo vya dola aliwatoa kwa nguvu
wananchi akitumia askari mgambo kupiga wananchi, kuchoma nyumba,
kuharibu mazao na halikadhalika kuwafungulia wananchi mashtaka.
Alitaja
maeneo mengine yenye migogoro kuwa ni wananchi na wawekezaji kuwa ni
Rufiji, Kilombero, Bagamoyo, Kisarawe, Muheza, Pangani, Katavi ,Meatu,
Kinondoni, Njombe na Ngorogoro.
Moto wa hoja hiyo uliwafanya
baadhi ya mawaziri kuinuka kuchangia akiwamo, Waziri wa Ardhi na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Tibaijuka, Waziri Nchi ofisi ya Waziri
Mkuu, (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu na Waziri wa Nchi ofisi ya
Rais (Mahusiano), Steven Wassira.
Akichangia hoja hiyo, Waziri wa
Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Tibaijuka alikubali kufanya
marekebisho katika sheria ya ardhi ili iweze kuwanifaisha watanzania.
Alisema
hakubaliani na hoja ya Mbunge Mdee ya kutaka kusitisha utoaji wa ardhi
kwa wawekezaji akisema hali hiyo inaweza kuleta matatizo zaidi.
Profesa Tibaijuka alisema ni aibu kwa nchi yenye ardhi kubwa na yenye rutuba kushindwa kujitosheleza kwa chakula.
Hivyo, alisema kuwapa wageni wenye mitaji
ardhi kwa ajili ya kilimo kutasaidia kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao
na hivyo kujitosheleza kwa chakula.
Profesa Tibaijuka alisema ili
watanzania waweze kunufaika na uwekezaji mkubwa wa ardhi nchini,
Serikali itakuwa inachukua hisa katika mshamaba hayo na kuziuza kwa
wananachi.
“Serikali hii haiwezi kukukbali wananchi wake kuporwa ardhi na wawekezaji,” alisema.
Alisema anakubalina kufanyiwa marekebisho sheria hiyo ili iweze kumsiadia mwananchi.
Waziri
Nagu, alisema hatuwezi kusitisha uwekezaji kwa wageni kwa sababu
itasabisha kurudisha nyuma maendeleo katika sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment