Wanajeshi wa Nigeria wanaendeleza operesheni kali ya kuwasaka wapiganaji wa Boko Haram katika eneo la Maiduguri Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wanajeshi hao wanatumia magari ya kivita na wanapewa usaidizi zaidi na helicopta za kijeshi.
Jeshi la Nigeria limedai kuwa limemuua kamanda mmoja mwandamizi wa Boko Haram Ibn Saleh Ibrahim.
Raia wa eneo hilo wamesema kuwa idadi kubwa ya watu wameuawa kwenye operesheni hiyo.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema Ibn Saleh Ibrahim aliuawa wakati wa makabiliano makali ya riasi wakati alipokuwa na walinzi wake sita.
Maafisa wa ulinzi nchini Nigeria wanaamini kuwa Bwana Saleh, alihusika na mauaji ya Generali mstaafu Mohammed Shuwa mwezi uliopita.
Kundi hilo la Boko Haram, ambao limeua raia wengi tangu mwaka wa 2009, halijasema lolote kuhusiana na kifo cha kamanda huyo.
Historia ya Boko Haram
Mwanzilishi wa kundi hilo, Mohammed Yusuf, aliuawa na maafisa wa ulinzi mwaka wa 2009.
No comments:
Post a Comment