Rais avunja serikali
Rais wa Ivory Coast
Rais wa Ivory Coast Alassane
Outtara amevunja serikali yake kufuatia mzozo kuhusu sheria mpya ya ndoa
itakayowapa wanawake haki sawa na waume zao.
Chama cha rais Ouattara, kiliunga mkono sheria hiyo, lakini viongozi wa upinzani waliopo serikalini waliupinga.
Chama
cha PDCI, kilichomuunga mkono Bwana Ouattara, katika uchguzi wa
November 2010, uliokumbwa na utata, ndicho kilichotoa upinzani mkali.
Wadadisi wanasema kuwa kutoelewana ndani ya
serikali ya nchi hiyo kunaangazia hali ya wasiswasi inayozidi kutanda
katika nchi hiyo inayokuza kakao kwa wingi duniani.
Hata hivyo, nchi hiyo inaendelea kuimarika
taratibu baada ya miezi kadhaa ya machafuko baada ya uchaguzi huo,
ambapo rais wa zamani Laurent Gbagbo alikataa kukukubali ushindi wa
Bwana Ouattara.
Aliyekuwa mgombea wa chama cha PDCI, Henri Konan
Bedie, alikuwa wa tatu kwenye uchaguzi huo, na alipomuunga mkono katika
awamu ya pili ya ughaguzi, Bwana Ouattara alimteua waziri mkuu kutoka
PDCI.
Lakini wandani wanasema kuwa Bwana Ouattara, kwa
sasa anaona kwamba haungwi tena mkono kikamilifu na PDCI, chama
kilichotawala Ivory Coast kwa miaka 39 tangu uhuru had mapinduzi
yaliyofanywa 1999.
Kama sheria nyingi barani Afrika, sheria za nchi
hiyo kwa sasa humpa mamlaka zaidi mume, akiwa kiongozi wa familia, naye
hupewa jukumu la kufanya uamauzi kuhusu maswala muhimu ya familia -
jambo ambalo chama cha Ouattara cha RDR kilitaka kubadlisha.
Amadou Gon Coulibaly, katibu mkuu katika ofisi
ya rais, alisema hatua hiyo ya ghafla la kuvunja serikali lilifanywa
baada ya PDCI kupiga kura na kupinga sheria hiyo mpya ya ndoa Jumanne
jioni.
Mpambe mmoja wa rais, aliyetaka jina lake
libanwe, aliliambia shirika la habari la AP kwamba: "Unaweza kusema kuwa
hili lilikuwa tone la maji lililosababisha maji katika jagi yafurike."
Tangu alipochukua hatamu za uongozi mnamo Machi 2011, Bwana Ouattara amesimamia kuboreka kwa uchumi nchini Ivory Coast.
Lakini hatua hizi zinatishiwa na mashambulizi ya
mara kwa mara dhidi ya vituo vya kijeshi na miundombinu nchini.
Inasemekana kwamba ni washiriki wa Bwana Gbagbo kutoka nchi jirani ya
Ghana wanaofanya mashambulizi haya.
Mnamo mwezi wa Septemba, mpaka kati ya nchi hizo
mbili ulifungwa wiki mbili baada ya shambulizi dhidi ya kituo cha
ukaguzi wa magari.
Kumekuwa na madai kwamba Bwana Ouattara hajitahidi vilivyo kujenga uwiano wa kitaifa kati ya wafuasi wake na wa Bwana Gbagbo.
No comments:
Post a Comment