Migomo yaanza ulaya
Maandamano Ulaya
Wafanyakazi katika mataifa
kadhaa ya muungano wa Ulaya wameandamana na kufanya migomo kupinga
kuongezeka kwa ukosefu wa ajira na mikakati ya serikali ya kupunguza
matumizi yake.
Migomo hiyo nchini Uhispania na Uturuki
imekwamisha shughuli za usafiri, biashara na shule na maafisa wa polisi
wamekabiliana na waandamanaji hao katika mji mkuu wa uhispania Madrid.
Kumekuwepo
pia na maandamano katika mataifa ya Ugiriki, Italia na Ubelgiji na
maandamano mengine yanatarajiwa katika mataifa mengine.
Safari za ndege nchini Uhispania na Ureno
zimefutwa ambapo mashirika ya ndege yametoa wito kwa wasafiri kuchunguza
ratiba ya usafiri kabla ya kuelekea katika viwanja vya ndege.
Migomo hiyo imeandaliwa na Chama cha wafanyakazi
barani Ulaya ETUC ambacho ndicho kinaongoza migomo hiyo inayotarajiwa
kushuhudiwa katika mataifa yote ya ulaya.
Mratibu wa chama hicho Judith Kirton-Darling
ameiambia BBC kuwa mipango ya kupunguza matumiza ya serikali haifanyi
kazi kwa kuwa raia wa kawaida ndio wanaoendelea kuteseka.
Jumla ya makundi 40 kutoka mataifa 23 yamehusika na maandamano yaliyofanyika hii leo.
Vyama vya wafanyakazi nchini Uhispania na Ureno
vilitangaza kuwa mgomo huo ambao ulianza saa sita za usiku kupinga
mipango ya serikali zao ya kupunguza matumizi , kuongezwa kwa viwango
vya ushuru, mishahara ya wafanyakazi, malipo ya uzeeni pamoja na huduma
zingine zikipunguzwa.
No comments:
Post a Comment