Wanajeshi kutumwa Baragoi
Polisi aliyejeruhiwa Baragoi
Rais Mwai Kibaki wa Kenya
ameidhinisha mpango wa kuwatuma wanajeshi, katika eneo la Samburu
Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo kufuatia kuuawa kwa maafisa wa polisi
na wezi wa mifugo ambao waliwavizia.
Takriban maafisa 42 wa polisi waliuawa, katika tukio ambalo limetajwa kuwa baya zaidi katika historia ya Kenya.
Baada
ya kuongoza kikao cha dharura la baraza la usalama, rais Kibaki
amesema, wanajeshi hao wametumwa katika eneo hilo kuwasaka wezi hao wa
mifugo na kujaribu kurejesha mifugo hiyo iliyoibwa pamoja na kuwapokonya
silaha.
Ripoti zinasema mamia ya watu wametoroka kutoka eneo hilo wakihofia mashambulio ya kulipiza kisasi.
Maafisa hao wa polisi walishambuliwa siku ya
Jumamosi iliyopita karibu na mji wa Baragoi wakati walipokuwa njiani
kuwafuata wezi hao wa mifugo.
Habari zinasema waliofanya mashambulio hayo walitumia silaha nzito kama vile mabomu ya kudungua magari na makombora ya gruneti.
Kiongozi mmoja wa kidini ambaye hakutaka jina
lake litajwe, ameiambia BBC kuwa wakaazi wa eneo hilo wanahofu kuwa
maafisa wa usalama wanaweza kuwanyanyasa wakati wa operesheni hiyo ya
kuwasaka walioendesha mashambulio dhidi ya maafisa wa polisi.
Eneo hilo hukaliwa na watu wa jamii ya Samburu
na Turkana ambao mara kwa mara huibiana mifugo na kugombea maeneo ya
malisho ya mifugo.
.
No comments:
Post a Comment