Jamaa za waathiriwa wa mkasa huo watambua maiti
Moto umezuka tena katika jengo la ghorofa lenye viwanda kadhaa vya kutengeneza nguo katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka.
Msemaji wa polisi alisema moto huo uliotokea Jumatatu ulianza katika orofa ya tatu ya jengo lenye orofa 12,kwa mujibu wa shirika la habari la AFP lilisema.
Moto huu umezuka siku mbili baada ya kiwanda kingine nje ya Dhaka kuteketea na kuwaua zaidi ya watu 100.
Maelfu ya wafanyakazi kutoka kiwanda cha nguo cha Tazreen waliandamana Jumatatu, wakidai wapewe mazingira bora zaidi ya kazi.
Walisema kwamba watu wengi walikwama ndani ya jengo, katika moto huo uliozuka jioni Jumamosi, na kuongezea kwamba jengo hilo lilikuwa halina milango inayotumika kunapozuka moto.
Hali duni ya usalama
Moto wa Jumatatu ulianza katika kiwanda cha nguo cha Euro-Bangla mnamo 10:05 asubuhi (04:05 GMT), maafisa walisema.
"Unaonekana kama moto mkubwa sana. Makundi ya wazimamoto wameshawasili na wanajitahidi kuuzima," afisaa mmoja wa kuzima moto wa ngazi ya juu aliiambia AFP.
Duru zinasema kwamba takriban watu wanane walijeruhiwa.
Wazimamoto wajitahidi kuzima moto
No comments:
Post a Comment