Uvutaji sigara ni hatari kwa ubongo kulingana na wanasayansi nchini Uingereza
Kuvuta sigara “kunaozesha”
ubongo kwa kuathiri vibaya kumbukumbu, uelewa wakati wa masomo na uwezo
wa kushauriana. Hii ni kulingana na wachunguzi wa King’s College, nchini
Uingereza.
Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya
miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito kupita kiasi pia
ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.
Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.
Wachunguzi nchini Uingereza walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya shtuko wa moyo na kiharusi.
Shirikisho la kuhamasisha kuhusu ugonjwa wa
Alzheimer, unaoathiri ambavyo watu wanakumbuka mambo, ulisema: "Sote
tunafahamu ya kwamba uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu,
kipimo cha Cholesterol au kiwango cha juu cha mafuta mwilini, huathiri
vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote hivi pia
vinaathiri ubongo.
"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora,
wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo
la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
Kuvuta sigara “kwaozesha” ubongo kwa kuathiri
vibaya kumbukumbu, masomo na uwezo wa kushaurianana, kulingana na
wachunguzi wa King’s College, London.
Uchunguzi wa watu 8,800 wenye umri wa zaidi ya
miaka 50 ulionyesha kwamba shinikizo la damu na uzito uliopita kiasi pia
ziliathiri ubongo, lakini kwa kiwango cha chini zaidi.
Wanasayansi walisema ni sharti watu wajue kwamba hali ya maisha inaweza kuathiri vibaya ubongo pamoja na mwili.
Wachunguzi wa King's College walikuwa wanachunguza uhusiano kati ya hali ya ubongo, na visa vya mshtuko wa moyo na kiharusi.
shirikikisho la kuhamasisha ugonjwa wa
Alzheimer, unaoathiri kumbumkumbu, ulisema: "Sote tunafahamu ya kwamba
uvutaji sigara, kuweko kwa shinikizo la damu, kipimo cha cholesterol cha
juu, huathiri vibaya moyo. Uchunguzi huu unadhihirisha kwamba vyote
hivi pia vinaathiri uongo.
"Ni sharti watu wale chakula chenye lishe bora,
wawe na uzito wa kadri, wafanye mazoezi mara kwa mara, wapimwe shinikizo
la damu na cholesterol, na pia wasivute sigara."
No comments:
Post a Comment