Rais Obama awasili nchini Burma


Obama awasili Burma
Obama awasili Burma

Rais wa Marekani Barack Obama anaitembelea nchi ya Burma, akiwa rais wa kwanza aliyeko mamlakani wa nchi hiyo kufanya hivyo.

Makundi ya watu, wakipeperusha bendera za Marekani, walijipanga pembeni mwa barabara za Rangoon wakati Obama alipokuwa anaelekea kukutana na Rais Thein Sein.

Ziara hii inakusudia kuzipa msukomo harakati za mageuzi alizoweka Rais Thein Sein tangu utawala wa kijeshi ulipofika kikomo mnamo Novemba 2010.

Bwana Obama anategemewa kutangaza kitita cha dola milioni 170 kama msaada.

Akiongea katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok, mnamo Jumapili, Obama alisema kuwa ziara yake siyo ya kutia sahihi juhudi za nchi hiyo, bali ni ya kukiri kwamba kumekuwa na mageuzi kadhaa wa kadhaa. “Ni wazi kwamba Burma ingali inastahili kupiga hatua zaidi”.

No comments:

Post a Comment