Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amesema wakati umefika sasa elimu ya sekondari iwe bure ili kumwondolea mwananchi mzigo.
Lowassa aliyasema hayo jana mjini Babati kabla ya kuendesha harambee ya
ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa
Babati.
Jumla ya Sh. milioni 120 zilihitajika katika harambee hiyo ili kukamilika ujenzi huo baada ya kutumika zaidi ya Sh. milioni 186.
Gharama za ujenzi wa kanisa hilo ni Sh. milioni 600.
Katika harambee hiyo, Sh. 45,854,950 zilikuwa ni ahadi na taslim Sh. 87 540,480 na hivyo kufanya jumla ya Sh. 133, 895,430.58.
Lowassa alisema kwa sasa kila kata hapa nchini ina shule ya sekondari na
huo ulikuwa mpango wake akiwa Waziri Mkuu na alisimamia na kufanikiwa
kwa asilimia 100.
''Ni lazima tukubali na tujadili suala hilo kwa manufaa ya nchi kwa kila
Mtanzania kukubali ushauri huo wa elimu ya sekondari kuwa ya bure,"
alisisitiza.
Aliongeza kuwa serikali inapaswa kugharimia elimu ya sekondari bila woga
na mwananchi anapaswa kuchangia mahitaji mengine ikiwemo kupata elimu
ya kilimo kwanza kwani kilimo ndiyo uti wa mgongo wa nchi.
Aidha, Lowassa alisema wito wa Rais Jakaya Kikwete, wa shule za
sekondari kujenga maabara kwa wingi, unapaswa kuungwa mkono pia na kila
Mtanzania.
No comments:
Post a Comment