Rufaa ya Jerry Muro Februari mwakani
Rufaa
ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro na wenzake wawili waliokuwa
wakikabiliwa na kesi ya rushwa ya Sh. milioni 10 imepigwa kalenda
kusikilizwa hadi Februali 18 mwakani.
Jaji Dk. Fauz Twaibu wa Mahakama ya Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam,
alipiga kalenda rufaa hiyo baada ya upande wa Jamhuri kuomba
kuibadilisha.
Hata hivyo, ombi hilo halikuweza kupingwa na upande wowote wa mawakili
kwani pande zote ziliridhika na ombi hilo na zote zimekubali tarehe hiyo
iliyopangwa kwa ajili ya kusikilizwa tena rufaa hiyo.
Muro na wenzake waliachiwa huru na Hakimu Frank Moshi wa Mahakama ya
Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Novemba 13 mwaka jana baada ya upande
wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.
Mbali na Muro washtakiwa wengine walioachiwa huru ni Edmund Kapama maarufu kwa jina la Dokta na Deogratius Mgasa.
Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Februali mwaka 2010 upande wa mastaka
uliokuwa ukiongozwa na aliyekuwa wakili wa Serikali Boniface Stanslaus
ambaye ni marehemu kwa sasa.
Kutokana na kifo cha wakili huyo ndipo wakili wa kujitegemea Richard
Rwezengo alimwakilisha Muro na wakili Majura Magafu akamwakilisha
mshtakiwa wa pili na wa tatu.
Awali ilidaiwa kuwa Januari 28 mwaka 2010 jijini Dar es Salaam
washtakiwa wote na wengine ambao hawakuwepo Mahakamani walikula njama na
kutenda kosa la kuomba rushwa.
No comments:
Post a Comment