Uganda imethibitisha kuwepo kwa Ebola
Virusi wa Ebola
Maafisa afya nchini Uganda
wamesema kwamba watu watatu wamekufa baada ya kuugua ugonjwa wa Ebola,
lakini serikali haina uhakika kuhusu kilichosababisha visa hivi
vilivyotokea Luweero.
Inashukiwa kuwa watu wengine watano
wameambukizwa,wawili kati yao wametengwa katika wodi maalum katika
hospitali kuu ya Mulago, mjini Kampala.
Hii ni mara ya tano kwa kuzuka kwa Ebola nchini humu katika miaka 12 iliyopita.
Mlipuko wa ugonjwa huo mnamo Julai mwaka huu ulisababisha vifo vya watu 17.
Inakadiriwa kuwa watu 17 waliaga dunia magharibi mwa Uganda, kutokana na ugonjwa huo mwezi Julai mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na
mipaka la Medecins Sans Frontieres (MSF), hakuna maafa yoyote
yaliyoripotiwa kuhusiana na ugonjwa huo hatari tangu mwezi Agosti.
Waziri huyo wa Afya ameliambia shirika la habari
la AFP, kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa watu hao waliaga
dunia kutokana na ugonjwa huo wa Ebola katika eneo la Luwero, takriban
kilomita sitini kutoka mki mkuu Kampala.
Lakini amesema mwanaume mmoja kutoka eneo hilo,
pia aliaga dunia mwezi uliopita, kutokana na kile kilionekana kuwa
dalili za ugonjwa huo, lakini hakuna uchunguzi uliofanyika kuhusiana na
kifo hicho.
Watu watano ambao ni jamaa wa karibu wa walioaga
dunia, wanaendelea kuchunguzwa na madaktari. Wawili kati yao wamelazwa
katika chumba maalum katika hospital kuu ya kitaifa ya Mulago mjini
Kampala.
Hakuna tiba maalum inayojulikana ambayo inaweza
kutumika kutibu ugonjwa huo, lakini wagonjwa hupewa dawa za kawaida za
kinga pamoja na zile za kupunguza maumivu na kutibu Malaria ili kuongeza
kinga mwilini.
Asilimia Tisini ya watu wanaogunduliwa kuwa na
virusi vinavyosababisha ugonjwa huo wa Ebola huaga dunia, na katika
kipindi cha miaka Kumi na mbili iliyopita kumekuwa na visa kadhaa vya
mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda.
Takriban asilimia 50 ya yatu 425 ambao walikuwa wameambukizwa virusi hivyo waliaga dunia mwaka wa 2000.
Wizara ya Afya, pamoja na Shirika la Afya
Duniani walikuwa wametangaza kwamba ugonjwa huo ulikuwa haupo tena
Uganda. Lakini umezuka tena.
Wanaougua Ebola hupata homa kali, huvuja damu, na viungo vyao vya mwili vya ndani huacha kufanya kazi.
Waganda wengi wanashangaa ni kwa nini nchi yao
hukumbwa mara kwa mara, lakini serikali inasema kwamba ni kwa sababu
mifumo yao ya uchunguzi imeboreka zaidi.
Hali kadhalika, katika mwezi mmoja uliopita watu
tisa wamefariki baada ya kuugua ugonjwa wa homa unaoambukiza wa
Marburg, unaofanana na Ebola.
No comments:
Post a Comment