Waasi wadungua ndege ya Khartoum

Mapigano Kordofan Kusini
Waasi katika jimbo la Kordofan
Kusini, nchini Sudan wanasema kuwa wamedungua ndege ya kijeshi karibu na
mpaka wake na Sudan Kusini.
Msemaji wa kundi la SPLM-North amesema kuwa
ndege hiyo ilidunguliwa kufuatia ufyatuaji mkubwa wa risasi katika eneo
la milimani la Nuba siku ya Jumatano.
Hakuna tamko lolote kutoka kwa serikali ya Khartoum kuhusu shambulizi hilo.
Waasi wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Sudan katika eneo hilo tangu Juni mwaka jana.
Mzozo huu wa Kordofan Kusini pamoja na Ule wa jimbo la Blue Nile umewafanya maelfu ya watu kutoroka makwao.
No comments:
Post a Comment