Wanajeshi watuhumiwa kuwajeruhi raia
Wanajeshi wa Kenya
Maafisa wa matibabu wamesema
watu kumi na watano wakiwemo wanafunzi watatu wamepigwa risasi na
kujeruhiwa mjini Garissa Kaskazini Magharibi mwa Kenya.
Majeruhi hao walipigwa risasi na wanajeshi
waliovamia shule hiyo na kuanza kuwapiga na kuwazuilia watu, baada ya
wanajeshi watatu wa Kenya kuuawa na watu wasiojulikana hapo jana.
Vituo vya kibiashara, shule na ofisi za Serikali zimefungwa huku wanajeshi hao wakipiga doria katika barabara za mji huo.
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Yusuf Haji ameiambia BBC kwamba hakuidhinisha hatua hiyo ya wanajeshi.
Afisa mkuu wa kimatibabu anayesimamia, hospitali
kuu ya mkoa mjini Garisa, Dkt. Musa Mohamed, ameiambia BBC kuwa watu 45
wamelazwa katika hospital hiyo, wawili kati yao wakiwa na majeraha ya
risasi.
Mapema hii leo, hospitali hiyo pia ilipokea watu wengine kumi na watano wakiwemo wavulana watatu.
Mmoja wao alikuwa na mareha ya riasi na wanaendelea kupokea matibabu.
No comments:
Post a Comment