Ajinyonga kukwepa dola baada ya kumcharanga mke mapanga

Mkazi wa kijiji cha Hamkoko Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, amejinyonga baada kumjeruhi vibaya mkewe kwa kumcharanga mapanga akihofia mkono wa sheria.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu, alimtaja aliyejinyonga hadi kufa kuwa ni Lucas  Magafu (63), na mwili wake ulikutwa ukining'inia  kwenye tawi la mti kijijini Hamkoko.

Mwanaume huyo anadaiwa kuwa siku moja kabla  ya  kujinyonga, alimcharanga kwa mapanga mkewe Lucia Mushi (49), akimtuhumu kufanya mapenzi nje ndoa yao.

Majeruhi huyo ambaye ni mwalimu katika Shule ya Msingi Msekwa, kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya mjini Nansio akiendelea na matibabu.

No comments:

Post a Comment