Mtoto
Gift Mustafa (4) mkazi wa Yombo Buza wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam, ameuawa kikatili na baba yake baada ya kumkatakata kwa panga
wakati akigombana na mkewe.
Tukio hilo lililotokea juzi majira ya saa 1:00 usiku eneo la Buza na
kuvuta umati mkubwa wa watu baada ya kuzuka ugomvi baina ya baba yake
mzazi aliyejukulikana kwa jina la Mustapha Mchele (37) na mkewe (mama wa
mtoto huyo) aliyejulikana kwa jina la Zulfa Mathias (23).
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Gift alipigwa mapanga mara kadhaa
ikiwamo kichwani na usoni hadi ubongo ukatawanyika na kufariki papo
hapo.
Mashuda hao wanaotaja umri wa mtoto kuwa ni miaka saba, walidai kuwa
aliporejea kutoka chuo (madrasa) alisikia baba na mama yake wakigombana
na aliita: “Baba baba akitaka kuamualia ugomvi huo,”
Hali hiyo ilimfanya baba yake aliyekuwa na panga kumgeukia na kumcharanga mapanga.
Mashuhuda hao walisema kuwa ugomvi wa wanandoa hao ulikuwa umechukua muda mrefu.
Mashuhuda hao walieleza kuwa, mbali na mtuhumiwa kufanya mauaji hayo,
pia alimjeruhi mkewe kwa panga hilo sehemu za mkononi na paji la uso.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo,
wananchi waliamua kujichukulia sheria mkononi dhidi ya yake kabla ya
polisi kufika eneo la tukio na kuwatawanya kwa kufyatua risasi hewani na
kufanikiwa kumwokoa.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke,
Englibert Kiondo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa
mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.
Kamanda Kiondo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali
ya Wilaya Temeke, na kwamba mama mzazi wa mtoto huyo amepata matibabu na
kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Alisema kuwa taarifa ambazo wamezipata kutoka kwa majirani, chanzo cha
mkasa huo ni matatizo ya kifamilia, na kusema kuwa polisi bado
wanaendelea na uchunguzi.
Kwa upande wao Hospitali ya Temeke walishindwa kutoa taarifa kuhusiana
na mwili wa marehemu ambao ulikuwa umehifadhiwa katika Hospitali hiyo
baada ya kurushiana mpira kati ya Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo na Ofisa
habari.
Awali Ofisa habari wa Hospitali hiyo,Joyce Nsumba
kupata ufafanuzi juu ya sehemu alizopata majeraha marehemu kabla ya
kufariki dunia, lakini alisema kwa wakati huo hakuwa na taarifa kwani
alikuwa nje ya ofisi na kumtaka mwandishi asubiri awasiliane na Mganga
Mkuu ili kupata taarifa kamili.
Hata hivyo alivyotafutwa kwa mara ya pili alisema atatoa taarifa baada uongozi wa hospitali hiyo kukaa kikao.
No comments:
Post a Comment