Shirika
linalowawakilisha mahakimu wa Misri limetangaza kuwa wanachama wake
hawatoisimamia kura ya maoni ya rasimu ya katiba itakayofanyika wiki
mbili zijazo.
Taarifa hiyo ya muungano huo wa mahakimu,
inajiri baada ya kuwepo mvutano kati ya mahakama ya juu nchini Misri na
wafuasi wa rais Morsi wenye itikadi kali za dini ya kiislamu.
Mahakama ya kikatiba imetangaza kuwa
inasitisha shughuli zake kwa muda usiojulikana baada ya mahakimu wa
mahakama hiyo kuzuiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa baraza rasimu hiyo
ya katiba.
Upinzani unasema rasimu inashusha hadhi ya uhuru wa watu.
Makundi ya upinzani yaliitisha maandamano dhidi ya kura ya maoni juu ya katiba hiyo itakayofanyika siku ya Jumanne.
Walisema kuwa Rais Morsi alivunja ahadi ya kutoitisha kura ya maoni bila ya makubaliano ya wengi kuukubali wito huo.
"vuguvugu la National Salvation Front, linapinga
kitendo kilichofanywa na ambachio hakikubaliki katu cha kuitisha kura
ya maoni juu ya rasimu ya katiba ambayo imekataliwa na watu
wengi''ilisema taarifa ya muungano wa vyama vaya upinzani kwa umma.
Upinzani unaamini kuwa rasimu hiyo inabana uhuru muhimu wa watu kikatiba.
No comments:
Post a Comment