Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli
UJENZI wa Barabara ya Kilwa, jijini Dar es
Salaam ambayo Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alikataa kuipokea mwaka
2011, baada ya kujengwa chini ya kiwango, umekamilika.Ujenzi wa kipande
hicho cha kilomita 5.1 kutoka Mtongani hadi Mbagala Rangi Tatu,
ulikamilika jana baada ya magari kuruhusiwa kutumia barabara bila
vikwazo vilivyokuwapo wakati wa ujenzi.
Mafundi wa Kampuni ya
Kajima waliokuwa wakijenga kipande hicho cha barabara, jana walionekana
wakiwa katika hatua za mwisho za kusawazisha udongo katikati ya barabara
hiyo yenye njia nne.Msongamano wa magari ulikuwa ukiwasababishia
usumbufu watumiaji wa barabara hiyo inayounganisha Dar es Salaam na
mikoa ya Lindi na Mtwara, sasa umekwisha.
Magufuli alikataa
kuipokea barabara hiyo kutoka katika Serikali ya Japan, iliyotoa msaada
wa fedha na ujenzi kufanywa na Kampuni ya Kajima, baada ya kujiridhisha
kuwa ilijengwa chini ya kiwango.
Magufuli alimweleza Balozi wa Japan
nchini, Masaki Okada kwamba asingeipokea barabara iliyo chini ya kiwango
hata kama imetolewa kama msaada kwa Tanzania.
Baada ya msimamo huo wa Serikali, Japan ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa kampuni hiyo ilijenga barabara hiyo chini ya kiwango.
Kutokana
na hali hiyo, Balozi Okada aliahidi kurudia ujenzi wa kilometa 5.1
kipande ambacho waligundua kuwa kampuni hiyo ilijenga chini ya
kiwango.Kazi ya ujenzi huo ilianza Juni mwaka huu.
Baada ya kauli
hiyo ya Balozi, Dk Magufuli alimtaka mkandarasi huyo kuondoa tabaka la
lami na kuweka tabaka jingine gumu lenye sentimita saba jambo ambalo
limetekelezwa baada ya marudio.Ujenzi wa Barabara ya Kilwa yenye urefu
wa kilomita 13.5 kutoka bandarini hadi Mbagala Rangitatu ulizinduliwa
kwa kuwekwa jiwe la msingi na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment