Usafiri Ubungo ni balaa tupu
Kituo cha mabasi Ubungo
WAKATI abiria wanaendelea kulalamikia kupanda
kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani, hali ya usafiri katika Kituo Kikuu
cha mabasi Ubungo imezidi kuwa mbaya.
Hali hiyo imekuja kutokana na kuwapo kwa
abiria waliokwama kuelekea mikoa ya kaskazini na nyanda za juu kusini
kutokana na uchache wa mabasi.
Mwananchi lilishuhudia abiria wakiwa wamekwama
kituoni hapo bila ya kupata ufumbuzi kuhusu safari zao huku wakiwatupia
lawama wamiliki wa mabasi, kuwa ndio chanzo cha usumbufu wanaoupata.
Walidai kuwa wamiliki hao wamekuwa wakifanya
makosa na hatimaye kufungiwa kwa kampuni zao hali inayosababisha kuwapo
kwa uhaba wa mabasi.
Wakizungumzia usumbufu huo, baadhi ya abiria
walisema hali hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa abiria wengi wanaokwenda
mikoani kwa ajili ya sherehe za mwisho wa mwaka.
“Sisi tuko hapa
kituoni tangu asubuhi na bado hatujapata uhakika wa safari kwani abiria
ni wengi, ikichangiwa na uhaba wa magari uliojitokeza kwa sasa, tunapata
usumbufu wa kuja kituoni na kurudi nyumbani,” alisema mmoja wa abiria
hao.
Abiria huyo aliyetajitambuliasha kwa jina moja
la Jesca alidai kuwa baadhi ya kampuni zinazomiliki mabasi hayo,
zimekuwa zikifanya makosa ya mara kwa mara ambayo yanaweza kuepukika na
matokeo yake, wanajikuta wakifungiwa kutoa huduma.
“Kuna makosa mengine yasiyo ya lazima ambayo
yanaweza kuepukika ni vyema kampuni miliki zikachukua tahadahari napema
ili kuepuka adha unayo tukumba,” alisema Bibi Jesca
Abiria waliokwama
katika kituo hiko ni wale wanosafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda
mikoa ya Tanga, Moshi, Arusha na mikoa ya Iringa na Mbeya.
No comments:
Post a Comment