Mwenyekiti wa Muungano wa
Afrika, Thomas Boni Yayi, ametoa wito wa kutuma vikosi kusaidia
wanajeshi kupambana na makundi ya wapiganaji nchini Mali.
Wapiganaji hao ambao wanajumuisha wale wa Tuareg, wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi.
''Mzozo wa Mali ulikuwa kitendawili
cha kimataifa na NATO inapaswa kusaidia kama ilivyo saidia
Afrghanistan,'' alisema Thomas Boni Yayi
''Hata hivyo, harakati dhidi ya wapiganaji hao zinapaswa kuongozwa na kikosi cha Afrika,'' aliongeza kusema bwana Yayi.
Mwezi jana Umoja wa Mataifa uliidhinisha mipango ya kutuma takriban kikosi cha wanajeshi elfu tatu nchini Mali.
''Bila shaka tuna wasiwasi kuhusu hali na hofu
ya kuendelea kuwepo makundi ya kigaidi katika eneo hilo , inaleta
wasiwasi kwa kila mtu kimataifa''
Maafisa wa UN wanasema kuwa hawakutarajia wanajeshi hao kutumwa huko kabla ya mwezi Septemba.
Bwana Yayi, ambaye ni rais wa Benin,alitoa wito wake baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper mjini Ottawa.
"NATO inapaswa kuchukua jukumu lake katika mzozo
huu, na kwamba kikosi cha Afrika kitatoa mwongozo, sawa tu na hali
ilivyokuwa nchini Afghanistan,''
Wanachama kadhaa wa NATO ikiwemo, Marekani na
Ufaransa, wako tayari,kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afrika
watakaoshiriki katika harakati hizi za kumaliza uasi, ingawa
hawajajitolea kutuma vikosi.
Bwana Harper alisema kuwa Canada , ambayo ni mwanachama wa , Nato, haijatafakari zaidi kuhusu kujihusisha kijeshi nchini Mali.
No comments:
Post a Comment