CHUKUENI TAHADHARI NA UTAPELI KWA NJIA YA SIMU
MTU
mmoja ambaye hajafahamika jina amekuwa na tabia ya kutapeli watu kwa
kutumia simu ambapo amekuwa akijifanya ni mtu unayemfahamu na huomba
msaada wa fedha.
Mtu
huyo ambaye anatumia namba 0714 530 869 na 0716 494 259 amekuwa
akijitambulisha kwa jina la mtu unayemfahamu sana na hutoa taarifa kuwa
simu yake ina matatizo kidogo hivyo kukuomba umtumie kiasi fulani cha
fedha kwa kuwa ana matatizo na yupo mkutanoni.
Aidha,
tapeli huyo hataki kabisa uongee naye bila shaka kwa kujua kuwa
utamtambua na badala yake hukuomba uwasiliane naye kwa njia ya sms.
Mara
nyingine atakuambia kuwa ana mgonjwa na mtumie fedha kwa namba ya
mjomba wake. Atakupa ahadi pia kuwa ukimtumia hizo fedha, atazirejesha.
UKITUMA TU, UMEUMIA. Chukueni tahadhari. Katika ofisi za mtandao huu
ametuma sms kwa wafanyakazi wengi lakini ameambulia patupu! Namba moja
(inayoishia 259) ameisajili Tigo Pesa kwa jina la LWITIKO MWANJOKA
lakini nyingine hajaisajili. Wizi anaoutumia ni wa kijinga sana, lakini
naamini kati ya watu 20, angalau 2 huwapata! Mjulishe na mwenzio,
usitume fedha kwa mtu usiyemjua, hata akitumia jina la mzazi wako!
No comments:
Post a Comment