Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki Mch. Clement
Fumbo akitangaza Halmashauri mpya ya kanisa hilo itakayokaa madarakadi
hadi sinodi ya mwaka 2014
HALI si shwari tena katika Kanisa la Moravian
Jimbo la Misheni Mashariki kutokana na Mwenyekiti aliyesimamishwa
uongozi na Mkutano Mkuu wa Jimbo (Sidodi), Mchungaji Clement Fumbo
kujichukulia madaraka na kutangaza uongozi wake mpya.
Fumbo alitangaza uongozi huo juzi katika ibada
iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Ushirika wa Tabata akieleza kuwa
uongozi wa juu wa kanisa unamtambua kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kanisa
katika jimbo hilo la Misheni.
Wakati hayo yakijiri sintofahamu imebakia kwa
waumini kuwa hivi sasa waufuate uongozi upi wa mwenyekiti
aliyesimamishwa na sinodi ama Makamu Mwenyekiti Sauli Kajura aliyepewa
mamlaka ya kuliongoza jimbo hadi kipindi cha mkutano mkuu wa uchaguzi
utakaofanyika mwaka 2014.
Kutangazwa kwa uongozi huo wa kanisa kumejiri
wakati pia kesi ikiendelea katika Mahakama ya Kisutu ambapo Mchungaji
Fumbo alifungua kesi ya kupinga uamuzi wa Sinodi akieleza kuwa
hakuhusika na upotevu wa Sh 500m hali iliyosababisha avuliwe uongozi huo
kupitia sinodi ya dharura.
Akielezea hisia zake kwa waumini wa Ushirika wa
Tabata, Mchungaji Fumbo alisema ameamua kuunda uongozi mpya wa jimbo ili
shughuli za kitendaji zisiweze kuendelea baada ya makamu mwenyekiti
,katibu na miongoni mwa wajumbe wa Halmashauri Kuu kusababisha mpasuko
kati ya waumini na wachungaji.
Mchungaji Fumbo alisema Juni 5, mwaka 2012
yalifanyika mapinduzi ya kumwondoa madarakani yeye watendaji, na baadhi
ya Wakristo kutengwa huku wachungaji wakitishiwa maisha kinyume na
taratibu za kanisa hilo.
Alisema jambo hilo lilisababisha mgawanyiko ndani
ya kanisa kwa ngazi ya viongozi na kuambukiza wachungaji na walei wa
kanisa la jimbo hilo hata kwenye majimbo mengine ambayo yana masilahi na
jimbo hilo.
Fumbo alisema Kanisa la Moravian Duniani
(COUF)kupitia kwa mwakilishi wake umeingilia kati na kutuma ujumbe wake
ambao ulikuwa Novemba 25,26, na 27 mwaka 2012 kwa lengo la kutafuta
kiini cha mgogoro ili kupendekeza suluhisho lake.
“Katika mikutano yake ya tume iliona njama za
makusudi za kumpindua mwenyekiti kwa njia isiyo halali kwa sababu
zisizojulikana, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na Katiba ya Kanisa la
Moravian (COUF) na katiba ya Jimbo la Mashariki,”alisema na kuongeza:
“Kutokana na hayo tume imeagiza yawepo mazungumzo
ya pande mbili yanayolenga kurudi kwenye mfumo wa uongozi wa mwaka 2010
na kufuata taratibu za mambo yaliyosababisha kukosa maelewano na
uchunguzi wa kina ufanyike kubaini kiini cha tatizo,”alisema Fumbo.
Alisema msuluhishi wa Kanisa la Moravian Duniani
(COUF) alinyimwa ushirikiano kutoka kundi la Makamu Mwenyekiti na Katibu
wake ambapo hawakutaka kusuluhishwa ili mgogoro umalizike.
Alisema kwa kuwa kanisa linahusu imani za watu kwa
kuzingatia kwamba uongozi uliochaguliwa mwaka 2010 ukiwa chini ya
mwenyekiti Fumbo haujamaliza muda wake mwaka 2014 ambapo ukizingatia
yalifanyika mapinduzi ya kuondoa baadhi wa viongozi wa jimbo hilo
(HAIJAMALIZIKA)
No comments:
Post a Comment