MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia
MWENYEKITI wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema
yaliyomkuta kwenye yake ziara mkoani Mtwara ambako amelazimika
kuikatisha, yametokana na umbea aliouita ni wa mwaka 2013.
Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, alisema hayo jana kwenye Ofisi za Bunge Dar es Salaam.
“Unasemaje (anamuuliza mwandishi), ngoja
nikwambie kilichotokea kimetokana na umbea tu wa mwaka mpya 2013, wewe
tambua hivyo na sitazungumza lingine zaidi,” alijibu kwa kifupi
akionyesha kukwepa kulizungumzia suala hilo zaidi.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini viliripoti
kuhusu Mbatia akiwa na wabunge wa chama chake, Moses Machali (Kasulu
Mjini ) na Agripina Buyogela (Kasulu Vijijini) walilazimika kujifungia
ndani ya ofisi za NCCR- Mageuzi wilayani Mtwara Mjini.
Hatua
hiyo ilifuatia baada ya baadhi ya wananchi kuamua kumrushia chupa tupu
za maji, huku wakimfuata kabla ya kuizingira ofisi hiyo wakiimba nyimbo
za kumshtumu kuwa ni mamluki.
Ilielezwa kuwa, hali ilikuwa tete eneo la
ofisi hiyo hasa baada ya giza kuingia, kwani wananchi walianza kurusha
mawe juu ya ofisi hiyo na wengine kujaribu kuvunja mlango na kurusha
vitu vinavyodiwa kuwa ni baruti zinazotumika kuvulia samaki .
Hali hiyo ilisababisha polisi waliofika kumuokoa kutumia mabomu ya machozi.
Mapema mwaka huu baadhi ya wananchi wa Mtwara waliandamana wakipinga gesi kusafirishwa kuletwa Dar es Salaam.
Badala yake, walitaka mtambo wa kuzalisha umeme kujengwa mkoani humo.
No comments:
Post a Comment